Yemi Eberechi Alade, Ghen Ghen Babe na binti waki Yoruba

Malkia wa kupendeza, kiongozi wa kucheza, malkia wa kuimba, muuaji wa biti, muiba nyoyo,na anaechukua pumzi. Yemi Alade, oooo!

Zaidi ya watazamaji milioni 3 kwenye Youtube lakini bado hajajua yuko wapi Johnny wake na ni mwaka 2017.

Vijana wanajiuliza wataanzaje kumnunulia Ferrari, Wasichana wanashangazwa na mambo yake makubwa anayoyafanya na staili yake ya muziki.

Kumbuka mwaka jana alitaka kumfanya msanii Nyashinski wa Kenya alie baada ya kuimba vizuri nyimbo aliyoiimba ya Mungu pekee(Alipigwa na butwaa lakini usimtajie suala la kulia)

Wakenya wanalimtaka, wa Nigeria wamemshikilia vita huko Twitter haiishi, lakini Yemi Eberechi Alade, Ghen Ghen Babe na binti waki Yoruba Ibo hawezi kukaa chini. Ametuweka katika ramani yake na nyimbo zake mpya na kolabo zake zinazotamba kila kona ya dunia.

Kwenye Coke Studio Africa, hajaja kucheza, amekuja kupendeza na amefanikiwa.

Msimu huu, tegemea mitindo mikali ya kiAfrika. Tegemea mitindo mikali ya nguo za kiAfrika na marembo ya uso. Shikilia pumzi yako kwa kuwa unatazama Coke Studio Afrika msimu wa tano(5).

Kaeni kwenye siti mumtazame Yemi Alade.