Vitu vitano unapaswa kufahamu kuhusu Izzo Bizness

Ni kijana mwenye swaga na na anayekua kwa kasi Zaidi kwenye umaarufu. Izzo bizness anaipeleka Tanzania kwenye levo nyingine ya Hip-hop. Sauti yake halisi na  video zake zimempeleka hadi kwenye Holi la heshima la Afrika. Tunasubiri kwa hamu kusikia ni kitu gani ameleta ndani ya Coke Studio Afrika  msimu huu.

Kwahiyo tafuta kiti ukae huku ukinywa Coka ya baridi kabisa , hivi ni vitu vitano ulivyokuwa huvijui kuhusu Izzo Bizness.

Mwite Kamau

Wazazi wake walimpa jina la Emmanuel, jina lake la jukwaani ni Izzo lakini aliamua kujichagulia jina la Kamau alipokuja nchini Kenya. Na jinsi nilivyotokea ni kama maajabu tu, na bado tunaendelea nae.

Anampenda Jay Z

Kuanzia Kichwani hadi miguuni, style zake zimechanganywa za Mbeya na Brooklyn, Huyu Kijana mwenye tabia za jiga anasema kwamba ni Mbeya pekee katika Afrika nzima unaweza kuiona Brooklyn.

Alianza kuimba akiwa Secondary

Akiwa kijana mdogo katika shule ya sekondari mjini Mbeya, Izzo Bizness alianza kuimba.

Anasema ‘Mwanangu, walimu walipokuwa wakinikuta narap walikua wananipa adhabu’’ hiyo haikutosha kuweza kumfanya akatize ndoto zake. Aliweza kuendelea na kuwashukuru mastaa kwa hilo.

Anajiamini

Mwaka 2013, Izzo Bizness akiwa mdogo aliandika “Mimi ni Ninja kutoka mtaani, natoka ardhi ya Mwalimu”

Miaka mbele ya baadae rapa aliyekuwa mdogo kaingia ndani ya Coke Studio Afrika akiwa mtu mzima na mwenye ndoto.

Ni shabiki mkubwa wa Bongowood

Izzo Bizness ni shabiki mzuri wa BongoWood, Tasnia ya movie nchini Tanzania, haijatokea bado lakini ana hakika itabadili mitazamo yetu na kuonyesha makuzi ya shujaa huyu. Vidole vimefungwa.

Kwa sasa tunakunywa vinywaji vyetu kuangalia muziki mpya wa kijana kutoka Mbeya ,nenda.