Rayvanny kuwa msaani pekee wa Afrika Mashariki kuwania tuzo za BET mwaka huu

Msanii utoka Tanzania anayehisiwa kama msanii anaekua kwa haraka Zaidi barani Afrika kwa sasa. Rayvanny anajulikana kwa ngoma zake kali kama vile ‘’Zezeta,Kwetu,Natafuta kiki na Salome aliyoshirikiana na Diamond Platnumz. 2017 umekuwa ni mwaka wa Rayvanny. Baada ya kuwa msaani pekee wa Afrika Mashariki kuwania tuzo za BET mwaka huu, Rayvanny alitajwa kuwania tuzo ya International Viewers Choice award. Hii yote imetokea wakati Rayvanny akiwa kwenye akirekodi shoo ya Coke Studio Africa. Ameongelea uwepo wake kwenye shoo ya mwaka huu: “Ninafuraha sana kuwa hapa kwasababu ilikuwa ni ndoto kuwa hapa! Mtegemee vitu vizuri” akaongeza “Shukrani kwa Coke Studio Africa – Muziki unatukutanisha pam0ja”

Ndani ya Coke Studio, Rayvanny anaungana na Dji Tafinha kutoka Angola. Rayvanny  yupo tayari kuialika Afrika kwenye utengenzaji wa Muziki. Anasema “Dji anakubali kipaji change – amekuwa kama kaka yangu sasa” ameongeza “Natamani tungetoa wimbo tuliofanya sasa hivi” Muziki aliofanya na Dji Tafinha pia utapigwa live na bendi noma ya Coke Studio. Shoo hii itarushwa ndani ya nchi 30 za Afrika na kwa mara ya kwanza Septemba 2017.

Rayvanny pia ameshiriki kwenye sehemu maalum ya Coke Studio Africa “The Global Fusion Edition” akiwa na mgeni wa Coke Studio wa kimataifa – Star wa pop toka Marekani Jason Derulo. Hii ni kama miujiza, Rayvanny amesema “Shukrani kwa Coke Studio Africa kuwa kunileta hapa. Nilisisimka sana niliposkia nitafanaya kazi na Jason Derulo” ameongezea “Sikutegemea yeye kuupenda muziki wangu pamoja na sauti yangu lakini muziki umetuleta pamoja”. Jason Derulo na Rayvanny walikutana tena pamoja nchini Marekani  kwenye tuzo za BET mwaka 2017. Wawili hao waliingia studio na tutegemee mengi zaidi yatakuja mwaka huu.

Rayvanny yupo chini ya lebo ya muziki – WCB iliyoanzishwa na Diamond Platnumz. Amesema kwamba boss wa lebo hiyo anajivunia maendeleo yake: “Diamond anajivunia sana kuwa na mimi, alipost hadi picha Instagram na kusema WCB milele na inanifanya nijisikie furaha.”

Rayvanny pia ni baba wa mtoto wa kiume. Anaongea kuhusu familia yake: “Mimi ni baba sasa wa mtoto wa kiume, jina lake ni Jaiden pia napenda sana watoto hivyo kumpata ni kama ndot imetimia.” Mbali na Muziki, Rayvanny anapendelea upishi “Napenda kula, na msosi ninaupenda ni Ndizi Nyama.”