MAFIKIZOLO KWENYE MIAKA 20

Kundi kongwe la muziki nchini Afrika Kusini la Mafikizolo linalounganishwa na Theo Kgosinkwe na Nhlanhla Nciza wanaaingia ndani ya Coke Studio mwaka 2017, wakishirikiana na rapa Nyashinski. Wakati wa Kipindi cha Coke Studio Afrika katika mahojiano mubashara kutoka Instagram baina ya wakongwe hawa wa ngoma ya Khona, Theo wa Mafikizolo alizungumzia kuhusiana na jinsi walivyokuwa na mambo waliyopitia walivyokuwa ndani ya Coke Studio Afrika na safari yao kwa muda wa miaka 20 kwa ujumla.

JINSI AMBAVYO MAFIKIZOLO ILIVYOANZA

Kundi hilo lilianza ambapo Theo alikuwa na ndoto ya kuwa muandishi wa nyimbo. Anasema “Kiukweli sikuwahi kutaka kuwa mwanamuziki lakini nikaona njia pekee ya kunifanya niweze kutambuliko ni kuwa kwenye kundi na ndipo nilipokutana na Nhlanhla kwenye mashindano ya vipaji na ndio nikamuuliza kama tunaweza kuanzisha kundi na hivo ndivo kundi lilivyoundwa”.

JINSI YA KUTOA NGOMA ITAMBULIKE

Na ngoma zao zilizohit kama vile Ndihamba nawe, Chelete, Happiness na Kucheza, Mafikizolo wanahusishwa kuwa ni moja kati ya waandishi wazuri wa nyimbo barani Afrika. Theo anaongea na sisi huku akisema ‘ Nilipokuwa nakua nilikua napenda sana kusikiliza nyimbo za watu wengine na nilikuwa nikitamani kuandika za kwangu mwenyewe. Nilikuwa nanunua muziki na kujaribu kutafuta aliyoitengeneza hiyo nyimbo ni nani. Watu kama Babyface walinihamasisha kuwa kama wao, nilipokuja kwenye tasnia hii nilikutana na Nhlanhla kwahiyo ningeweza kuanzisha bendi na kuwa muandishi, ni ngumu sana kuwa muandishi hapa Afrika kwasababu ni ngumu kufanya hiyo kazi na kufanya ndio kipato chako. Japokuwa kuna watu wanakwenda kusomea uandishi wa muziki na kujifunza jinsi ya kuandika ngoma zitakzotoka, viitikio lakini inakuwa  nzuri  inapokuwa halisi.

NDANI YA COKE STUDIO

Muungano wa Mafikizolo na Nyashinski utakuwa unatengenezewa biti na msanii mkubwa Afrika Kusini Sketchy Bongo, Theo anasema Tupo ndani ya studio toofauti na kwenye mazingira ya kiubunifu . Tunapendelea na vizuri kuwa hapa’ Anaongeza ‘’Tumefanya upelelezi kuhusiana na Nyashinski na kufahamu kuwa ni mtu makini na anayependa muziki. Sisi pia ni makini kwahiyo tunategemea tunaweza kufanya ngoma ya Hip-hop, Afro Beat , House au au yoyote tutakayotengenezewa.

SIRI YA KUDUMU KWAO

Mafikizolo wanasema kuwa walihamasishwa na Miriam Makeba , Brenda Fassie, Lucky Dube na Yvonne Chaka Chaka na wasanii wengine kutoka nje ya Afrika, Wakiwa ndani ya Coke Studio Mafikizolo walitangaza kuwa ndani ya mwaka 2017 wataachia Albamu maalumu itakayokuwa na nyimbo 20 mwaka huu wakiwa wanasherehekea miaka yao 20 ndaniya tasnia ya muziki. Wanasema siri kubwa ya kudumu katika muziki ni kushirikiana na wasanii wengine na lugha nzuri pia.

Hiyo inaleta rangi nzuri kwenye muziki, japokuwa mashabiki hawaelewi lugha tofauti. Ni muhimu kwa wasanii kusahau wao ni kina nani, unaweza kujua wewe ni nani ukitaka kufanikiwa kwenye biashara ya  muziki.