Mafanikio ya AKA

“Nimekuwa nikifanya kazi kwa miaka mingi kufikia hapa. Albamu yangu imetoka 2011 karibuni miaka 7 sasa kwenye muziki pamoja na kolabo na wasanii kibao duniani” amesema AKA – the Supa Mega wa South Africa ambaye kwa sasa anasumbua na ngoma kama “The World is Yours” na “Caiphus Song”

AKA anatokelezea kwenye Coke Studio Africa 2017 akiungana na Mnaijeria Baddo aka Olamide ambaye anarudi kwenye shoo kwa mara ya pili. AKA anafurahia kushirikiana na mwanahiphop mwenzake. Anasema “Ni msanii mkubwa nchini kwake na barani Africa. Mashabiki wetu watakuwa na shauku ya kusikia kolabo yetu itakavyokuwa, na nategemea vile itakavyopokelewa.” Wawili hao watakuwa na produza kutoka South Africa – Sketchy Bongo.

Mafanikio ya AKA yanatokana na uwepo wake, jitihada na msukumo ulio ndani yake. “Najiona mwenye bahati na niliyebarikiwa kuwa kwenye nafasi hii. Kuwa na kipaji ni kitu kimoja na pia kuwa na kipaji na kubarikiwa ni kitu kingine. Ninathamini sana hilo.” Coke Studio Africa inamleta AKA kwa mara ya nne Nairobi. Ameshiriki matamasha mengi sana nchini Kenya – Moja wapo inayokumbukwa ni Blankets and Wine Festival ambayo alisema “Nairobi ni sehemu nzuri kwangu kwasababu watu wa hapa wanaupendo na muziki wangu na kuna mashabiki wengi wa muziki hapa”

Kwenye Coke Studio Africa mwaka jana AKA alikshirikiana na Mnaijeria mkali wa Dance hall Patoranking. Wimbo wao “Special Fi Mi” ulikuwa noma, na ulikwenda mpaka kwenye chati za Afrika na UK. Baada ya shoo, wawili hao walikwenda kufanya video ya wimbo. Amesema AKA, “Special Fi Mi ilikuwa moja ya nyimbo bora zilizotoka Coke Studio, tumefanya video kabisa na ni wimbo ambao nimefanya nao shoo nyingi nchini Africa nilipotemebelea”

Mwaka huu, Coke Studio imeunganisha Coke Studio Africa na Coke Studio South Africa. Olamide ambaye anatambulika kama rapa mkali Mnaijeria, amerudi Coke Studio Africa – 2017, tangu msimu wa tatu wa shoo ambapo aliungana na malkia wa Zambia wa Marrabenta Neyma uliotayarishwa na Legendari kutoka Kenya produza Musyoka.