Kutana Naye producer Gospelondebeatz

Tuna mtayarishaji nyota wa muziki GospelOnDeBeatz akizungumza na Coke Studio kwa mara ya kwanza kuhusu yeye na muziki wake.

Naitwa GospelOnDeBeatz lakini jina langu la kiserikali ni Gospe; Chinemeremu Obi. Ni produza wa muziki toka Naijeria na muandishi anayejulikana kwa kutengeneza nyimbo kama No Kissing Baby wa Patoranking na Sarkodie wakiwemo na wengine. Nilianza kupiga ngoma nikwa na umri wa maika 7 na kinanda nikiwa na miaka 9. Mapenzi yangu ya kupiga kinanda na kutengeneza midundo yalikuwa nilipokuwa nikitumbuiza mbele ya kanisa la wazazi na sehemu tofauti. Ujuzi wangu katika kuproduz muziki ulitambulika nilipokuwa na miaka 17 nilipotengeneza nyimbo kumi za albamu ya injili ya kwaya ya kanisa la wazazi wangu.

Nahisi dunia inaanza kutambua na kukubali muziki wa Africa. Kipindi cha nyuma tunachukua muziki wa watu wengine lakini nafikiri ni muda sahihi sasa tumeamua kuwa makini na kilicho chetu na kujivunia. Naamini kila kitu tunachofanya kinapelekea muziki mzuri, dunia itendelea kutambua muziki wetu kama ambavyo wamekwisha anza kuelewa. Hatupo pale tulipotaka kuwa lakini hatupo pale tulipokuwepo pia, hivyo tumeendelea.

Kwakuwa tuna muziki wa Mashariki, Magharibi na kusini- yote ni muziki wa Afrika. Bado tuna ladha na ladha hiyo ni tofauti na dunia ya Magahribi. Naamini uelekeo wa muziki na ni Afrobeat. Nataka kumfikia kila mmoja haijalishi ni wapi anatokea-  Naijeria hadi Kenya – fanya kila uwezacho na pia anga ni kikomo.

Kwenye mradi wa Coke Studio Africa, ntafanya kazi na Joey B na Amanda Black, kati ya wasanii wa Afrika na ilikuwa ni uzoefu mkubwa. Nimekuwa nikimfuatilia Mi Casa kwa muda mrefu sasa na nimefanikiwa kufanya nao kazi kwenye Coke Studio pia. Siwezi kuelezea nina msisimko wa aina gani. Coke Studio Africa ni sehemu sahihi ya kupata mzuka na kufurahi.