Kutana na Nasty C

Kutana na Nasty C. Kusema ni mdogo inategemea na mwaka gani ulizaliwa, na sio kitu kila mmoja angependa kuongelea, au sio? Kwa haraka haraka, Nasty C anafahamika kwa nywele zake mbaya, na hivi karibuni nywele zake mbaya zimezidi kukua.

Unaweza kwenda kwenye insta yake kuangalia, lakini kama wewe ni shabiki unajua kuwa hizi ni albamu zake.

Mdurban huyu ni muandishi wa nyimbo, rapa na produza. Mbali na kutokelezea kwenye Coke Studio, Nasty C ameshafanya makolabo makubwa na kutengeneza muziki mpya na marapa wengi wakali wa Africa.

Amepokea tuzo ya mkali mpya wa mwaka- iliyomfanya awe msanii mwenye umri mdogo kupata tuzo ya Hiphop South Africa.

Ana tabasamu zuri, lakini ukisikiliza muziki wake utagundua kuna kitu zaidi kinaendelea

Aliulizwa mnyama gani anayemchagua kuwa, hasiti kabla ya kujibu kitu usichitegemea. Nyoka.

‘Sio kwa ubaya lakini. Wanasogea kimya kimya, lakini wakishambulia utakiona’

Jinsi anavyoongea inakufanya usisimke. Huyu jamaa si wa mchezo – na hana sababu ya kucheza.

Alianza Sanaa akiwa na miaka tisa. Na sasa ana umri gani?

’20. Nafanya yangu mzee’

Siri yake ya kutengeneza muziki mkali kila muda anapodondosha mdundo?

‘Sio kwamba nakaa chini na kupanga, naacha mabo yaende’

Akiwa na wimbo wake mpya 031 uliotoka iTunes, pamoja na kolabo na mnaijeria Runtown, itabidi uvae miwani ili kumtazama.

Moja ya watu aliokuwa akiwaangalia na kaka yake, aliyekuwa produza kipindi cha nyuma. Alikuwa akizunguka studio hatimaye kushinda hapo hapo, baadae kutengeneza wimbo wake wa kwanza. Pia anamuangalia AKA, ambaye anafurahi kufungua shoo zake.

Sasa kwa kufahamika huku, hakuna kisichowezekana kwa Nasty C.

Kaa tayari.