Eddy Kenzo Kuhusu Chimbuko

Eddy Kenzo ni aina ya mwanamuziki ambaye anavaa uhusika na kucheza upande wa furaha na upande wa Maisha ya kawaida ya mwananchi wa Uganda. Anahusika katika kutengeneza moja ya video yenye watazamaji wengi Africa Mashariki, Sitya Loss, ambayo pia imelitoa kundi la madensa linalojulikana kama Ghetto Kids. Kwenye Coke Studio Africa 2017, Edddy ameungana na Mghana Bisa Kdei. Anaongelea albamu yake mpya “BIOLOGY”, na kumbukumbu zake ndani ya Coke Studio:

Kuhusu Chimbuko

Baadhi ya ngoma zlizohiti za Eddy ni Stamina, Jubilation na Yanimba. Anasisitiza kwamba kufanikiwa kwenye tasnia ya muziki unakiwa kwa halisia. Anasema: “Wasanii wengi wa Afrika wanavutiwa na tamaduni nyinginezo lakini kuna sababu ya kwanini unaijua nchi yako zaidi. Kama ukibaki na uhalisia wako nakuimba ladha ambazo watu wako wataelewa- utafanikiwa”

Mabadiliko ya Tamaduni

Eddy Kenzo anasema kuonyesha utamaduni wa chakula kwenye Coke Studio ni sehemu muhimu ya shoo “ni muunganiko ambao hata sisi wasanii tunapata kuonja vyakula tofauti vya nchi tofauti. Mara zote ni vizuri kwa Waafrika kubadilishana tamaduni”

BIOLOGY - Albamu

Eddy Kenzo ameachia albamu yake. “Albamu yangu mpya ni baraka kwangu na Afrika Mashariki yote itaipenda kama vile furaha ya Maisha. Nimekua kama mtoto wa mtaani na ninajivunia nilipo leo hii. Watu wanataka tu kuwa matajiri lakini mimi nataka kuwa na furaha. Hu undo ujumbe wa albamu yangu. Ina nyimbo za mapenzi na mimi ni mtu wa muziki wa kufurahi hivyo kuna nyimbo za kucheza pia – na ni mmoja wa watu wanaopenda kufurahi”

Eddy kuhusu mapenzi na Muziki

Eddy amesema mapenzi yake kwa muziki na kuimba ni Maisha yake. Ameeleza: “Nikiwa studio au jukwaani kufanya shoo nakuwa na furaha kwasababu ilikuwa ni ndoto yangu. Natakiwa kuamka asubuhi kila siku kuimba kwasababu nisipofanya hivyo nitaumwa” ameongeza “Nafanya kazi kwa juhudi kuwa na Maisha mazuri na kufanya familia yangu ijivunie. Juhudi zinazaa matunda na ndio maana ninaongeza juhudi.”