Dakika Kumi na King Kiba

Muimbaji na muandishi wa muziki Alikiba maarufu kama King Kiba kama ambavyo mashabiki zake wanamuita, ni mmoja kati ya wasanii wakubwa Afrika Mashariki. Alikiba amekuwa msanii wa pili bara la afrika kusaini na lebo kubwa ya kimataifa ya Sony music Entertainment. Anasema nimekuwa nikisubiri kwa hamu na kutamani kuona muziki wa Afrika unapoelekea, nafikiri sasa ni muda wa sahihi kwa muziki wa Afrika kuiteka dunia, Alikiba vilevile amechaguliwa kama boss wa lebo  ya Rockstar 4000  moja kati ya lebo kubwa zinazosimamia wasanii Afrika.

Ana heshima kwa mashabiki zake sehemu zote ndani na nje ya nchi , Alikiba kwa miaka ya hivi karibuni ameweza kujishindia tuzo mbalimbali kama vile tuzo ya MTV Europe Music Award kama Msanii bora Afrika wa Mwaka., ingine ikiwa ni tuzo za MVP nchini Nigeria na nyingine tuzo za chaguo la watu ( People choice award) kama msanii bora wa kiume wa mwaka, zote hizo ikiwa ni mwaka 2016. Pia ni msanii wa kwanza Afrika Mashariki kuongoza kwenye jarida la Hiphop Magazine ‘THE SOURCE’ na Huffington post.

Wengi wanajiuliza siri ya Alikiba ni ipi . Anasema anaweza kutoa mapendekezo yake kwa mapenzi yakke ya muziki ndipo alipoanzisha safari yake ya muziki. Anasema ‘Nilipokuwa nina umri wa miaka mi5, ndipo nilipoanza kupenda muziki, nilianza kuimba na kucheza nikiwa nina miaka 7 na kuanza kuandika nyimbo

Baada ya kumaliza shule mwaka 2004, Alikiba aliandika nyimbo yake ya kwanza ya Maria na kuendelea kuachia nyimbo zingine baada ya hapo. Baadhi ni kama vile Najuwa, Ndugu wangu, Kuteseka , Namshukuru Mungu, Sabrina na Yatima. Albamu zake zikiwemo Cinderela ya mwaka 2008 na Ali K for Real ya mwaka 2009. Kiba pia ametangaza albamu yake kabla ya mwaka 2017 kuisha.

Kwa kuongezea tu manjonjo ya sauti yake, Alikiba pia ni mcheza shoo na pia ni muigizaji. Anaongea kuhusiana na vipaji vyake “Binafsi vinanipa furaha na hamasa. Sifa moja na zingine pia naweza kufurahia na kuvipenda sawa.

Alikiba pia alikuwa kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio Afrika  akishirikiana na mwimbaji Victoria Kimani kutoka nchini Kenya. Na prodyuza mkali Owuor Arunga aliweza kuwatengenezea nyimbo kama Loving You/Dushelele nyimbo ambazo waliziimba. Mfalme huyu amerudi tena kwenye shoo ya mwaka huu huu akishirikiana na mwanamuziki Patoranking kutoka nchini Nigeria. Kwenye shoo walitengenezewa na prodyuza Masterkraft, huku wakishirikiana pia na msanii Ozane maarufu kutoka nchini Togo. Kuangalia shoo hizi nenda kwenye www.youtube.com/CokeStudioAfrika