NATAKA KUFANYA COLLABO NA CHIDINMA: BEN POL ASEMA

Misago Kasago | NEWS | 7 January, 2016

 

Msanii wa Tanzania Ben Pol azugumza kuhusu mafunzo alizopata Coke Studio Africa alipofanya mash up na Wangechi, rapper wa Kenya. Soma alichojifunza akiwa Coke Studio Africa Season III.

R&B superstar Ben Pol ameongelea muda wake akiwa Coke Studio Africa, recording nchini Kenya nakusema amebahatika kukutana na Chidinma, msanii kutoka Nigeria (aliyefanya mash ups huu msimu na group kutoka Kenya: Elani) na wamekuwa na maongezi ya kufanya chochote.


Ben Pol akielezea kufanya kazi na Chidinma anasema; "Tumekuwa tukiwasiliana mara kwa mara, tunatumiana voice note na kuongea mambo ya muziki, tukiwa tayari muda wowote basi kuna kitu tunaweza kufanya."

Wasanii wengine ambao Ben anasema amekutana nao ni pamoja na producer Silvastone, ambaye hivi karibuni amefanya kazi na Ace Hood wa Marekani na Sarkodie wa Ghana. Ben anasema ameongea naye kuhusu kufanya wimbo pamoja.

Ben Pol alivyokuwa Coke Studio Africa pia alikutana na Sauti Sol, wasanii wa Kenya ambao maarufu wao unajulika ulimwenguni. Katika Coke Studio Africa Season III, walifanya mash ups na wasanii wa Nigeria: Yemi Alade na Ice Prince Zamani. Ben Pol pia aliweza kufanya collabo na Avril na Nameless, akiwa Kenya.

Kuhusu wazo la nyimbo zake kufanyiwa mash up, Ben Pol anasema yeye ni msanii anayeweza kufanya mambo mengi ndio maana ilikuwa rahisi kupokea wazo la mash up na kufanya kazi Coke Studio Africa. Ben pia ameamini kuwa mash up za nyimbo zake zimefanya nyimbo zake ziwe bora zaidi.

Tazama Tena Ben Pol Coke Studio Africa Showcase

Akiongelea mapokezi ya mash up zake kwa mashabiki wa muziki Tanzania Ben Pol anasema; "Mashabiki wamenishangaza kwa comment zao nzuri walizoandika chini ya kila mash up niliyofanya, mrejesho ni mzuri sana, watu wengi hawakutegemea kuwa nyimbo zangu zinaweza kuongezewa utamu."

Kuhusu alichojifunza kutoka Coke Studio Africa season III, Ben Pol anasema msanii wa kimataifa ni muhimu sana uwe na show bora iliyopangwa.

Ben anasema; "Kuanzia show, mavazi, wasaidizi wa kuimba, muonekano wa stage na movement ya msanii vimepangwa na watu. Muziki wako unapangwa na director wa muziki."

 

Misago Kasago
Kuafata @CocaColaAfrica