YARED NEGU

Yared ni moja ya wasanii wenye sauti zinazokimbiza kwenye muziki wa pop nchini Ethiopia, akivuka mipaka ya aina za muziki na mipaka ya nchi akiwa na lengo la kuupeleka muziki wa Ethiopia utambulike dunia nzima. Mkali huyu anayetamba na wimbo wa “Adimera” ametengeneza jina kubwa kama mnenguaji na mwimbaji na anafahamika kwa shughuli pevu akiwa jukwaani. Yared atakuwepo kwenye Coke Studio Africa 2019, akiwa na mwimbaji kutoka Uganda King Saha, wakiwa na produza mkali Daddy Andre (Uganda).

 

CAREER

Kipaji cha muziki cha Yared kilianza kuonekana mwaka 2015 alipoachia ngoma yake ya kwanza ‘’Yebelegn’’. Ikifuatiwa na “Yemerkato Arada” mwaka 2017, iliyopata kuchezwa mno Ethiopia na kwingineko. Mkali huyu ameendelea kutoa Nyimbo 8 baada ya hapo. Zikiwemo ‘’Zelelaye’’, ‘’Hulumu Agere’’ na ‘’Chemere’’— zote zikiwa zinakubalika kwa upekee machoni mwa watu. Yared kwa sasa anaifanyia kazi albamu yake. Kwa miaka amekuwa ni mwenye mafanikio kwa kutambulika na kushinda tuzo kama Best Single of the Year Award kwenye 9th Addis Music Awards.

 

MUSIC INTERESTS

Amefanikiwa kupafomu sehemu kubwa ya Ethiopia, Europe na Mashariki ya Kati, Ujuzi wa kuimba na kucheza wa Yared hujionesha akiwa jukwaani. Mbali na muziki pia amejikita kwenye harakati za haki za binadamu na kujitolea kusaidia watoto wanaoishi mtaani kutokana na matatizo tofauti.

 

BACKGROUND

Yared Negu alizaliwa na kukua mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Kabla ya umaarufu na heshima kubwa, alikuwa mnenguaji kwenye vikundi maarufu Kemise na Hahu. Baadae alijiunga na Ras Theatre, iliyoamsha ari yake ya muziki na kuwa njia ya kuingia kwenye tasnia ya uimbaji.