WINKY D BIO

Mnenguaji na mwimbaji wa kutoka Zimbabwe Winky D kwa sasa yupo juu kwenye muziki wa dance hall wa nyumbani. Ni mshindi wa mara 10 wa Zimdancehall Awards (amekuwa akishinda kuanzia mwaka 2008 hadi 2016). Anafahamika kwa aina yake ya kipekee ya reggae, dub, dancehall, na afro pop, mwimbaji huyu anafahamika kama Gafa, ameweza kuwakamta wapenzi wa muziki kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Akiwa na ngoma kama “Disappear” iliyobamba chati za shoo ya BBC 1Xtra, Winky ameonesha unguli wake kwenye muziki wa dancehall Zimbabwe. Anatimba ndani ya Coke Studio Africa 2019 akiwa na Messias kutoka Mozambique.


CAREER

Winky D alirekodi wimbo wake uliomtambulisha “Ndiri Rasta”, uliopokelewa vizuri na wapenzi wa muziki wa dancehall mwaka 2004 chini ya Blacklab Records, kwenye Luckspin Riddim. Mafanikio yake yameiweka dancehall ya Zimbabwe kwenye sehemu mpya. Akiwa na timu makini ikiwa na Bartholomew Vera, Jonathan Banda na kaka yake Layan Soljah, Winky D ameweza kuipeleka bendera ya dancehall juu na ngoma yake iliyobamba ya “Musarova Bigman”. Pia ameshinda tuzo tano za NAMA Awards (2011-2016), ZIMA Award mwaka 2016, Victors Award mwaka 2012 na Africa Entertainment Award mwaka 2011.


MUSIC INTERESTS

Winky D hutumia muziki kugusia masuala ya kijamii kumepaza sauti Zimbabwe, wakati huo huo akiufanya muziki wa dancehall ujulikane zaidi. Mkali huyu amepanda jukwaa moja na wakali wenye majina kama Sean Paul, Akon staa wa Jamaika Beenie Man.


BACKGROUND

Wallace Chirumiko alizaliwa Kambuzuma, Harare. Alianza kujihusisha na muziki akiwa na umri mdogo, alipoanza kukusanya kaseti na santuri za reggae. Alipofikisha miaka 16 alipafomu kwaenye tamasha la Ghetto Lane Clashes event lilikuwa likiibua MaDj. Kuanzia hapo aliingia kwenye tasnia na kukuza jina kwa kuonesha kipaji chake mbali na umri wake. Ujuzi na heshima yake vilimpa jina la 'Wicked Deejay', ambapo sasa amelifupisha kuwa Winky D.