VALTER ARTISTICO

Valter Artístico ni mwimbaji na mtunzi kutoka Mozambique na ni mmoja wa mastaa wanaokuja kwa kasi na sasa anatamba na Nyimbo kama “Marandza”, “Chefe do Quarteirao”, “Nandzzicado”, na “Nasci Pra Te Amar” akimshirikisha Twenty Fingers. Yupo ndani ya Coke Studio Africa 2019 kwenye Big Break segment akifanya kolabo na Rudeboy (Nigeria) na Khaligraph Jones (Kenya), huku wakali hawa wakiwa chini ya produza Mkenya Magic Mike.

CAREER 

 

Alianza kama rapa akiwa na kundi la Universe Rappers, alibadilika na kufuata mtindo wa Kizomba ambapo aligundua na kufanya aina nyingine ya muziki. Valter aliingia rasmi kwenye tasnia ya muziki mwaka 2013 na kutusua kuingia mainstream alipoachia ngoma yake iliyotamba “Sou Feliz”, akishirikiana na Cizer Boss mwaka 2016. Mwaka mmoja mbele alichaguliwa kuwania tuzo ya Best Upcoming Artist at the Africa Entertainment Awards.

 

MUSIC INTERESTS

Akivutiwa na stori za kimaisha, maumivu, na hisia za mapenzi, Valter’s ni mkali mwenye kipaji cha kipekee cha uandishi. Akiwa na Nyimbo kibao, anaendelea kuachia ngoma juu ya ngoma na kujikusanyia mashabiki wengi Mozambique.

BACKGROUND

Valter Ricardo Mandlate a.k.a Valter Artistico alizaliwa April 17, 1996 Maputo, Mozambique. Tangu utotoni, mkali huyu mwenye miaka 22 amekuwa akipenda kuimba na ameendelea na tasnia kama rapa na mwimbaji. Amesainiwa na Game Over Entertainment, umaarufu wake unazidi kukua.