SKALES

 

Ukitaja wasanii wa Nijeria waliopeleka mbele muziki wa Afrobeats mkali wa Naijeria Skales na listi yake ya ngoma zilizobamba kama “Shake Yo Body” lazima umtaje. Akiwa na zaidi ya ngoma 250 chini ya jina lake, Skales amefanya vizuri kwenye tasnia kwa zaidi ya miaka 10 sasa, na ameshirikiana na wakali wanaokiki duniani kama Wizkid, Major Lazer, Davido, Tiwa Savage, Olamide and Nicki Minaj. Muziki wake ni mchanganyiko wa pop, Afro Pop, na rap. Mkali wa “Booty Language” yupo ndani ya Coke Studio Africa 2019 ambapo atapafomu na mkali toka Tanzania Nandy, na kolabo lao litasimamiwa na Mnaijeria GospelOnDeBeatz (Nigeria).

 

CAREER

 

Kwa sasa amesainiwa na Baseline Records, Discography ya Skales ya ngoma zilizobamba na kuiteka Afrika ni kama “Currency” aliomshirikisha Davido, “Agolo”, “Temper” na Burna Boy, pamoja na “Fire Waist” akishirikiana na Harmonize. Alikuwa sehemu ya  “Run Up” - Afrosmash remix ya Major Lazer pamoja na Party Next Door, Yung L, Chopstix na Nicki Minaj. Skales hadi sasa ameachia albamu tatu; Man of The Year (2015), Never Say Never (2017) na Mr. Love (2018). Albamu mpya yenye ngoma 16 ikishirikisha wasanii kama Sarkodie, Rwanda's Neza, na  Cassper Nyovest kutoka South Africa.

 

MUSIC INTRESTS

 

Muziki umefanya Skales kupafomu kwenye majukwaa makubwa duniani. Novemba 2018 alipafomu kwenye tamasha la One Africa Music Fest Dubai akiwa na rapa wa Marekani Fabulous na mastaa wengine wa Africa. Ni Mnaijeria wa kwanza kuwepo kwenye tamasha kubwa la reggae beach fest nchini Dubai pamoja na Kymani Marley. Kwa kuongezea, Skales amefanya shoo UK, Canada, Ethiopia, Seychelles, Uganda na baadhi ya miji ya US kupitia Empire Mates Entertainment US Tour. Pia alitokea kwenye tamasha la mwaka 2013 la Felaberation, kwaajili ya lejendari Fela Kuti.

 

BACKGROUND

 

Raoul John Njeng-Njeng alizaliwa mwaka April 1991, Skales alikulia Kaduna, Nigeria. Mapenzi yake ya Muziki yalionekana alipokuwa akishinda kwenye stoo ya kaseti ya mama yake. Alisoma University of Jos na baadae alihamia Lead City University, ambapo alihitimu shahada Office Management and Technology. Wakati akiwa University of Jos alishiriki mashindano ya Zain Tru Search competition na kushinda mashindano ya North Central region edition. Mwaka 2008, Skales alianza kuingia kwenye tasnia ya muziki kwa kuachia ngoma kama  “Must Shine” na “Heading for a Grammy”. Mwaka mmoja baadae alisainiwa na Banky W’s Empire Mates Entertainment (EME) kabla hajaondoka mwaka 2014 na kuanzisha lebo yake OHK Music. Anasema kuwa kuwepo Coke Studio Africa ni moja ya ndoto zake kubwa kwenye muziki wake hadi leo.