RUDEBOY

Mkali toka Naijeria Rudeboy aka King Rudy ni moja kati ya wakali wanaoheshimika na wenye ushawishi Afrika. Akiwa kwenye tasnia kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa njia ya wasanii wapya kama sehemu ya kundi la muziki P-Square na kama solo. Kwa sasa anashikilia chati na ngoma kama “Together” akimshirikisha Patoranking, “Somebody Baby” na “Reality”, mwandishi huyu mwenye kipaji anaendelea kutengeneza ngoma kibao zinazokiki Afrika. Mkali huyu yupo ndani ya Coke Studio Africa 2019 akiwa na mkali wa Hiphop Kenya Khaligraph Jones. Wawili hawa watakuwa na produza Mkenya Magic Mike.

 

CAREER

Mwimbaji, mwandishi na produza aliyesainiwa chini ya lebo ya Rudeboy Records alianza muziki akiwa kwenye kundi la P-Square. Alianza kufanya muziki kivyake mwaka 2017 kwa kuachia ngoma mbili zilizofanikiwa: “Fire” na “Nkenji Keke”. Mwaka 2018, aliachia ngoma tano zikiwemo “Is Allowed” akimshirikisha Reminisce na “Together” akiwa na Patoranking. Akiwa mmoja wa P-Square, ametingisha chati za muziki Afrika kwa Nyimbo kama “Personally”, “Alingo” na “Do Me” pamoja na kuachia albamu sita. Umaarufu wake barani Afrika umempatia tuzo kadhaa kama: Artist of the Year kupitia Kora Awards (2010) na Best Group kupitia MTV Music Africa Awards (2009).

 

MUSIC INTERESTS

Akiwa na mashabiki wengi duniani, Rudeboy amezunguka kufanya shoo barani Ulaya mwezi July 2018 ambapo alipafomu miji 10 kwa zaidi ya mwezi mmoja. Amezunguka na kupafomu kwenye shoo zilizojaza US na Rwanda. Alikuwa kama msaani wa kushtukiza kwenye Coke Studio Koroga Festival (Kenya) Novemba 2018. Rudeboy amaefanya kazi na wakali kama Akon, T.I, Diamond Platnumz, Timaya, na wengine.

 

BACKGROUND

Paul Okoye, Rudeboy amekulia Nigeria na kusoma St. Murumba secondary school. Hapo ndipo alipokuza kipaji chake cha muziki kwa kujiunga na kikundi cha muziki cha shule na maigizo kisha kuanza kuimba, kucheza kama MC Hammer, Bobby Brown na Michael Jackson akiwa na kaka yake Peter. Baadae alijiunga na kundi la acapela quartet na kuunda kundi la “Smooth Criminals” mwaka 1997. Kundi hilo lilivunjika miaka miwili baadae na kuanzisha P-Square— ambalo litakumbukwa kama kundi la kwanza la mastaa wa pop Afrika.