RAYVANNY

Mwimbaji na mwandishi toka Tanzania Rayvanny hana shaka kuwa ni mmoja wa wakali walio juu Afrika kwa sasa. Kuibuka na ushindi wa tuzo ya International Viewer’s Choice award mwaka 2017 – inamfanya kuwa msanii pekee toka Afrika Mashariki kuonja utamu wa BET Award. Ngoma zake zilizofanya poa ni kama Chombo, Zezeta, Kwetu, Mwanza akiamshirikisha Diamond Platnumz, na Makulusa akiwa na DJ Maphorisa na DJ Buckz. Mwaka 2018, alishirikishwa kwenye wimbo wa Tip Toe wa Jason Derulo, aliyekutana nae kwenye Coke Studio Africa 2017 katika Global Music Fusion. Msimu wa Coke studio 2019, Rayvanny anarudi akiwa na Naiboi, produza Lizer.


CAREER

Rayvanny alijipatia umaarufu alipoanza kupafomu kwenye shoo za mkali Madee. Chini ya uongozi wa Tip Top connection na lebo ya Mkubwa wa Wanawe music pamoja na uangalizi wa Babu Tale, Rayvanny ameendelea kujenga jina lake na kuchukua mafunzo ya muziki. Kwa sasa amesaini na moja ya lebo kubwa Afrika Mashariki, Wasafi Classic (WCB). Alianza kuachia ngoma moja baada ya nyingine, Rayvanny amepafomu majukwaa mengi tofauti Tanzania kama Serengeti Fiesta, Kilimanjaro Music Awards na kampeni za uraisi za CCM (2010).


MUSIC INTERESTS

Kufuatia mafanikio ya wimbo wa Kwetu, wenye watazamaji Milioni 7 kwenye YouTube, Rayvanny ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani wakiwemo Diamond, DJ Maphorisa, Jason Derulo, Khaligraph Jones, Bahati na Queen Darleen. Kama mkali wa Bongo Flava, ubunifu wake kwenye muziki ni rahisi kukariri ambao umefanya apate watu wengi.


BACKGROUND

Jina lake ni Raymond Shaban Mwakyusa alizaliwa 1993, Rayvanny alionesha dalili za kupenda muziki akiwa shule. Alishinda mashindano ya Serengeti Fiesta Freestyle mkoani Mbeya mwaka 2011, na aliendelea kushinda mashindano ya kitaifa yaliyomuweka kwenye nafasi nzuri ya kimuziki. Hapo ndipo alipojulikana na Tip Top connection waliomchukua chini ya uongozi wao. Mengine yakawa historia.