MR EAZI BIO

Bila shaka ndiye msanii mkali wa kujitegemea kwenye muziki wa Afrobeats music scene, Mr. Eazi ameacha alama kama staa dunia nzima. Anafahamika kwa mahadhi yake ya Banku sound, amepiga kazi na majina makubwa kwenye tasnia kama Diplo, French Montana na Giggs. Mshiriki huyu wa tuzo za BET ameachia EP yake hivi karibuni ya “Life is Eazi Vol. 2 Lagos to London” mwaka 2018 to. Kwenye Coke Studio Africa 2019, staa huyu atatimba na kupiga shoo na Mtanzania Nandy na kundi la kenye la Ethic.


CAREER

Mr. Eazi alipata mafanikio kimataifa kupitia ngoma kama “Bankulize” kutoka kwenye mixtape ya “About To Blow”. Aliendelea kutoa ngoma zilizopata mashabiki kama “Skin Tight” akimshirikisha Efya, “Hollup”, “Dance for Me” na Eugy, “Leg Over” na “Pour Me Water”. Mnaijeria huyu anafahamika hadi UK, na aamewahi kuingia kwenye chati kwa kupiga makolabo na wakali kama RAYE kwenye “Decline”, “Bad” na Steel Banglez na “Bad Vibes” akimshirikisha M.O na Lotto Boyzz. “Decline” na “Bad Vibes” walishirikishwa kwenye 20 bora za chati za U.K huku “Bad” ikifika 40 bora.

Mwaka 2017, Mr. Eazi aliachia mixtape ya “Life Is Eazi, Vol. 1 - Accra to Lagos” – akitoa heshima kwa Nigeria na Ghana, nchi mbili zilizochangia muziki wa wake wamahadhi ya Banku. Mwaka 2018, alishirikishwa na Major Lazer kwenye wimbo “Tied Up” pamoja na Raye. Amepokea heshima mara kadhaa kwa miaka ikiwemo kuchaguliwa kushiriki tuzo za MOBO kama Best African Act mwak 2017, the Headies Award kwa Next Rated (2016), Top Naija Music Award kama Msanii wa mwka (2016) na Apple Music’s Up Next artist mwaka 2017.


MUSIC INTERESTS

Wakati anakuwa alisikiliza muziki tofauti kama Majek Fashek, Bob Marley, Madonna, Backstreet Boys na Ja Rule. Muziki wake umepitiwa mara milioni 250 katika mitandao ya kudownload, jina lakae bado linaendelea kukua. Mwaka 2018, Mr. Eazi alianzisha program ya emPawa Accelerator Programme – jukwaa la kisanaa kwaajili ya kukuza wasanii 100 wa muziki kila mwaka na kubadilisha maisha ya vipaji vya wasanii wasiosainiwa.


BACKGROUND

Amezaliwa Port Harcourt, Nigeria, Oluwatosin Oluwole Ajibade anajulikana zaidi kama Mr. Eazi. Familia yake ilihamia pembezoni kidogo mwa Lagos alipokuwa na umri wa miaka 4. Alipomaliza elimu ya Sekondari akiwa na miaka 15, Eazi alienda nchini Ghana kujiunga na elimu ya chuo kikuu mwaka 2007. Hapo ndipo Mr. Eazi alipopata ujuzi wa ujasiriliamali, alipoanza biashara ya kusafirisha na kuchimba madini kabla ya kurudi kwenye muziki.