LAYLIZZY

Laylizzy; Rapa wa Msumbiji mwenye tuzo zake na mwandishi wa nyimbo anayejulikana kwa ubunifu wake pale akichanganya lugha za Kireno na Kiingereza katika nyimbo zake. Nyimbo zake pendwa kama "Hello" na "Too Much" zilizoshirikisha wakali wawili wa hip hop ya Afrika Kusini: Kwesta na AKA. Anachukuliwa kama mmoja wa wasanii wa miji wa Mozambique wenye vipaji, wenye ujasiri, na uthubutu, Laylizzy anaweza kutawala kwa urahisi tasnia. Kwa mara ya kwanza kwenye Coke Studio Africa 2019 akiwa na Mganda Fik Fameica na Lizer, mtayarishaji wa muziki maarufu kutoka Tanzania.

 

CAREER

In 2015, alibadili jina kutoka Laylow hadi Laylizzy. Aliendelea kujitengenezea mashabiki kibao nchini Mozambique kwa kuachia mixtape kila mwaka, utamaduni ambao unawanufaisha wanaHiphop wa Zambia. Hadi leo na mixtape tano : “Dinheiro Limpo” (2010), “Unsigned” (2011), “Artistic” (2012), “Intelligent Ignorance” (2012), na“CallmeSirJeremias” (2013), Laylizzy anaendele kusogeza muziki wa Zimbabwe barani. Mwaka 2015 alisaini dili la record/management/publishing na Geobek Records & Entertainment, ambayo imekuza brand yake. Mkali huyu ametokea kwenye shoo tofauti akiwa na mastaa wengine wa rap kama Future, Cassper Nyovest, Preto Show na AKA.

 

MUSIC INTERESTS

Ushawishi wa awali wa Laylizzy katika muziki wa rap unatoka kwa vipaji kama Jay Z, Snoop Dogg, Dre Dre na Notorious B.I.G. Linapokuja eneo la muziki wa Afrika, ana sehemu yake na amesukuma brand yake zaidi ya mipaka ya lugha ya Kireno.

 

BACKGROUND

Edson Abel Jeremias Tchamo anajulikana zaidi kwa jina lake la hatua Laylizzy. Alizaliwa Maputo, Msumbiji mwaka 1988. Wakati wa miaka 14, Laylizzy pamoja na rafiki yake bora na mtayarishaji Ellputo walijiunga na kundi la muziki, 360 degrees. mwaka 2011, Laylizzy alihamia London kufuata shahada ya katika Sheria ya Biashara, wakati pia anatarajia kushughulikia mpango wa dili la kurekodi. Baada ya kuhitimu, Laylizzy alichagua kufuata ndoto yake ya kazi ya muziki.