KHALIGRAPH JONES

Anatajwa kama Rapa bora kwenye AFRIMMA Awards – 2018, Mfalme wa rap Kenya Khaligraph Jones a.k.a Papa Jones si wa kumtilia shaka kuwa ni mmoja kati ya marapa waanaotazamwa sana barani Africa kwa kipindi hiki. Anafahamika kwa michano yake ya haraka kama Twista’s au M.I’s, aina yake ya uchanaji bado ya kujiachia. Kimuziki, Khaligraph ameweza kutusua kwenye muziki tofauti tofauti, nyakati tofauti na mashabiki tofauti huku akikuwa kwa haraka hadi kufikia kuwa mmoja wa marapa wanaotazamwa. Kwenye Coke Studio Africa 2017, Khaligraph alikutana na mwimbaji wa Rwanda Bruce Melodie. Kwa mara ya pili atatimba ndani ya shoo na kushirikiana tena ndani ya Coke Studio Africa 2019 na Mnaijeria Rudeboy huku wakiwa na mtayarishaji Magic Mike wa Kenya.

 

CAREER

Hujivunia alipotokea Kayole, Nairobi - Khaligraph anatazamwa na wasanii wachanga kwenye gemu la rap, hasa wale wanaotokea mazingira kama aliyokulia. Leo ana nguvu na wafuasi na anatazamwa na kila mtu. Mwezi June 2018, aliachia albamu ya yenye ngoma 17 “Testimony 1990”, ambayo ilikuwa ni moja ya album zilizopakuliwa kwa wingi nchini Kenya kwenye mtandao wa Boomplay and iTunes.

 

MUSIC INTERESTS

Mbali na mafanikio ya albamu ya Khaligraph na makolabo kibao leo hii, kuna miaka mingi aliyoangaika na kukwama kwa mixtape kadhaa. Kuna zilizokaa kwa zaidi ya miaka mitano kabla ya kupata nafasi ya kuchezwa. Lakini hii haikumkwamisha Khaligraph kutumbuiza kwenye majukwa kama WAPI, ambapo alitajwa mara kwa mara kama mfalme wa kilinge cha Hiphop. Baada tu ya Khaligraph kuanza kupanda chati, alianza kuandaa lebo ambayo itawakilisha na kusaidia wengine. Ni kiongozi wa The Blu Ink Corp Record label. Pia ni mwanzilishi wa The Baba Yao Foundation CSR. Pia ameanzisha kilinge cha 'Khaligraph Presents' kuvumbua, kuendeleza na kutangaza vipaji vya vijana.

 

BACKGROUND

Safari ya Khaligraph kama msanii ilianza akiwa na umri mdogo na aliwatazama wasanii wa muziki tofauti na kusoma vitabu. Aliendelea kuweka mapenzi na hiphop/rap na pale nafasi ilipojileta ya mashindano ya The 2009 Channel 'O' MC Africa Challenge, akiwa na miaka 19 alishiriki na kuingia hadi fainali. Mashindano hayo ndio yalikuwa mwanzo wa Khaligraph Jones. Ameenda na msemo maarufu wa “Respect the OGs”- “Heshimu wakubwa” kwenye jina lake. Imekuwa ni msemo maarufu kwenye Hiphop ya Kenya uonatumika kumuongelea Khaligraph kama kumpa heshima.