HARMONIZE

Mkali wa Bongo fleva mwenye sauti tamu, Harmonize, aliyesainiwa chini ya lebo Wasafi Records (WCB) ni nguli ajaye, kiufupi ni mmoja kati ya wasanii wakubwa Africa mashariki kwa sasa. Ladha zake za kiafrika zinavyotamba kama  “Kwa Ngwaru” akiwa na Diamond Platnumz, “Fire Waist” na mkali wa Coke Studio Africa 2019 Act : Skales, remix ya ‘‘Sisi Maria” na Omoakin pamoja na “911” akiwa na Yemi Alade na Krizbeatz. Nyimbo nyingine zilizokiki ni ‘’DM Chick’’, “Bado”, “Niambie”, ‘‘Happy Birthday” na ‘’Show Me’’. Akiwa na zaidi ya watazamaji milioni 120 kwenye YouTube, Mkali huyu ana mashabiki wengi na atakuwepo ndani ya Coke Studio 2019, akishirikiana na mwimbaji kutoka Uganda Sheebah huku kolabo yao ikitengenezwa na produza GospelOnDeBeatz—legendari.

 

CAREER

Alianza kutusua mwaka 2015 baada ya kutoa ngoma iliyoitwa “Aiyola” ambayo mpaka sasa ina watazamaji zaidi ya milioni 10 kwenye YouTube. Maarufu kwa uandishi wake na Nyimbo zinazokaririka, Harmonize ameingia studio na wakali kibao wa Afrika wakiwemo Mafikizolo, Sarkodie, Eddy Kenzo, Korede Bello, Emma Nyra, DJ Neptune, OmoAkin and Jah Prayzah.

 

MUSIC INTERESTS

Mafanikio yake ya kishindo yameleta heshima na tuzo mara kadhaa. Kolabo yake ya mwaka 2018 “Kwa Ngwaru’’ akimshirikisha Diamond Platnumz ilikuwa ni video ya kwanza Afrika mashariki kufikisha watazamaji zaidi ya milioni 10 ndani ya mwezi. Mwaka 2016, alishinda tuzo ya “Best New Comer” ya Africa Music Magazine Awards (AFRIMMA), “Best African New Comer” pia kwenye WatsUp TV African Music Awards na “Best New Artist” kwenye Africa Entertainment Awards (AEAUSA). Pia muziki wake umeweza kumpeleka kwenye matamasha  mbalimbali duniani, ikiwemo tamasha lake lililojaza watu ndani “Dar Live” lililoitwa “Kusi Night” jijini Dar-es- Salaam, bila kusahau uwepo wake alipotokea kwenye Hard Rock Café in Las Vegas, USA.

 

BACKGROUND

Jina lake ni Rajab Abdul Kahali alizaliwa Octoba 1991 mkoani Mtwara, Tanzania. Alipofikisha umri wa miaka 18 ndipo alipoanza kuuchukulia muziki kwa makini, alijiandikisha kwenye jukwaa kubwa la kusaka vipaji la: Bongo Star Search. Japokuwa hakukiki kwenye shoo hiyo , alikuja kusainiwa na Wasafi Records, moja kati ya lebo yenye mafanikio makubwa nchini humo. Alitajwa na kituo cha MTV Base kama “Msanii wa kumwangalia” mwaka 2017, mpaka leo hii ameendelea kuwa juu zaidi.