GOSPELONDEBEATZ BIO

Gospel Chinemeremu Obi anajulikana kama GospelOnDeBeatz ni mmoja wa maproduza wakali Afrika wakutegemewa. Ni muanzilishi na mmiliki mwenza wa Flux Factory – kampuni ya burudani – na bendi kubwa ya muziki nchini Nigeria: Alternate Sound. Inayojulikana kwa kutoa ngoma zilizotamba kama “Mama Africa”, ya Yemi Alade na “No Kissing”  ya Patoranking bila kusahau “Sauce”  ya Sarkodie akimshirikisha Tekno na Patoranking, na “Run Am” with David na Peruzzi; Gospel ana siri ya utengenezaji wa ngoma zinazobamba kwenye vidole vyake. Mjuzi huyu, mwenye uwezo wa kupiga kinanda na anaejiweza pale akiwa jukwaani kutengeneza muziki, amerudi kwa mara ya pili ndani ya Coke Studio mwaka 2019. Kwenye shoo atakuwa akitengeneza makolabo kati ya mkali wa rege na dance hall wa Zimbabwe Winky D na chipukizi kutoka Mozambique: Messias Maricoa.
 

Akiwa na msaada kutoka kwa Bendi yake, Gospel amekuza jina lake kama produza wa kipekee na muongozaji katika utayarishaji wa muziki barani. Uwezo wake umeonekana kwenye ngoma zenye mafanikio Afrika zenye majina makubwa ya wasanii kama Praiz, Tiwa Savage, Iyanya, Burna Boy, Seyi Shay na MC Galaxy; zikichangia kwa hali ya juu kukua kwa majina ya wakali hawa barani. Uwezo wake wa kubadilika na kupiga midundo ya mahadhi tofauti ya muziki, inaonesha ukali na ubora wa kazi yake.
 

Kupitia jam sessions ya bendi yake , Alternate Sound, amepiga Nyimbo kama “Ojuelegba” ya Wizkid na “Oreo” ya Iyanya. Ameendelea kujihusisha na baadhi ya shughuli za kiburudani na anatazamwa sana katika kutoa ushauri kuhusu kutangaza wasanii na majukwaa ya kufanyia maonesho. Gospel kwa sasa anatengeneza film scores na montages, ikiwemo signature montage sounds kwaajili ya Taarifa ya habari vipindi vya Kakaki kupitia Africa Independent Television (AIT).
 

Amezaliwa Naijeria Mashariki, Gospel alianza muziki akiwa na miaka 7, alipoanza kuwa na mapenzi na ngoma. Alianza kupiga kinanda akiwa na miaka 9. Mapenzi yake ya kupiga kinanda  na kupiga midundo yalianza kukua miaka ya mbeleni, alianzia nyumbani na kwenye matamasha ya kanisani pamoja na matamasha ya kijamii. Ujuzi na ari ya utayarishaji wa muziki wa Gospel ulijionesha akiwa na miaka 17 alipotengeneza albamu ya Injili yenye nyimbo 10 ya Kwaya ya kanisa la wazazi wake. Ana Diploma ya Electronic Music Production, School of Audio Engineering (SAE) na Diploma ya Audio Engineering kutoka the Audio Institute of America (AIA).