FIK FAMEICA BIO

Rapa Fik Fameica a.k.a Fresh Bwoy’s kutoka Uganda mwenye aina ya muziki ya kipekee na mitindo ndio inayomfanya kuwa wakipekee. Nguli huyu mwenye ngoma kama “Property” na “Sitani Tonkema” ni moja kati ya marapa wanaokuja kwa kasi nchini Uganda, huku akiendelea kukua Afrika Mashariki na kwingineko. Mwaka 2018, alitajwa kama msanii bora chipukizi wa Uganda, msanii bora wa Hip-Hop na wimbo bora wa rap kupitia wimbo wake wa “Kutama” kwenye tuzo za mwaka za HiPipo Awards. Atakuwepo kwenye Coke Studio Africa 2019, pamoja na LayLizzy kutoka Mozambique; wawili hawa watatengenezewa mdundo na prouduza Lizer kutoka Tanzania.

CAREER

Ngoma yake iliyofanya vizuri mwaka 2015 iitwayo “Pistol ilimpelekea kuwa maarufu. Mwanzoni, muziki wake ulishika kumbi za starehe na chati za radio kupitia ngoma zake kadhaa kama “Mutuwulira”, “Stani”, “Byenyenya” na “Sconto”, ambazo zilimpa heshima na kutajwa kwenye tuzo. Alifanikiwa kushinda vipengele vya msanii bora wa Hip Hop wa mwaka, na msanii bora mpya Uganda kupitia Entertainment Awards, mwaka 2017. Pia ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kiume na msanii bora wa Hip Hop wa mwaka kupitia Buzz Teenies Awards. Pia amekuwa balozi wa nyumba ya mitindo iitwayo, the Abryanz brand house, Mitindo ya Fik ni moja ya vitu muhimu katika muziki wake. Pia kwa sasa ni balozi wa Africell telecom.

BACKGROUND

Walukkagga Shafiq aka Fik Fameica alizaliwa 1997 Kawempe, Kampala. Kwa zaidi ya miaka mitatu, “Fresh Bwoy” amafanikiwa kukua na kuwa mmoja wa wakali wa Hiphop Afrika Mashariki. Kubadilika kwake kama msanii kunaendelea kumuweka kwenye nafasi ya juu kwa mashabiki.