ALVIN KIZZ BIO

Bila ubishi huyu ni mmoja wa wakali wanaibukia nchini Uganda kwa sasa, Alvin Kizz anatajwa kama staa mkubwa ajaye Afrika Mashariki. Akiwa na Hit kama “Nkulowoozako”, “Tubalaba” na “Julia”, Alvin anaweza kuchukuliwa kama msanii mwenye uwezo wa kufanya mengi ambaye muziki wake umetokea kuvutia mashabiki mapema. Kijana huyu wa umri wa miaka 28 alifanikiwa kutusua mwaka 2018 na ngoma yake iliyotikisa iitwayo “Nkulawoozako” akiwa na diva wa Coke Studio Africa kutoka Uganda, Sheebah Karungi. Alvin pia atakinukisha ndani ya Coke Studio Africa 2019 kwenye kipengele cha Big Break, akipiga kolabo na Winky D (Zimbabwe) na Messias (Mozambique); wakali hao watatu watasimamiwa na produza Mnaijeria GospelOnDeBeatz.
 

CAREER

Alvin alianza kujishughulisha na muziki mwaka 2016 kupitia kolabo na staa na mwigizaji wa Uganda Hellen Lukoma kwenye “Ndagamutu”. Aliendelea kupiga kazi na wakali wa Uganda kama mnenguaji Ibra Buwembo, Dokta Brain, Roden Y, Fefe Bussi na Ykee Benda. Alvin kimkataba yupo chini ya the Team No Sleep record label, na Nyimbo zake anazoachia zinazidi kupaisha jina la lebo hiyo pia na kuuweka muziki wake kwenye chati za muziki.


MUSIC INTERESTS

Wasanii kama Tarrus Riley, Richie Spice, Fela Kuti na Oliver N’Goma ni wasanii waliomjenga Alvin kimuziki. Pia ni mtunzi mzuri wa muziki wa kuaminika. Kipaji chake cha uandishi kimetoa ngoma kali kama “Mummy Yo” ya Sheebah na “Manyi Go” wa Bebe Cool. Pia ameshiriki kuandika “Wankona” wa Sheebah.


BACKGROUND

Ruyonga Phillip Alvin kwa jina la kuzaliwa, alizaliwa mjini Katooke Kyenjojo, Magharibi mwa Uganda, Alvin Kizz leo hii anafahamika kama staa anayependwa Uganda. Ndani ya miaka miwili tu, jina lake limekuwa na kumpeleka kwenye jukwaa la Coke Studio Africa.