SHELLSY BARONET

Msanii mwenye vipaji mbalimbali nchini Mozambique, Shellys Baronet anafahamika kwa ngoma  yake ya Ultima Mocha  ambayo aliachia mwaka 2016. Ameingia ndani ya Coke Studio kwa mara ya kwanza mwaka 2017 akiwa kwenye kipengele cha BigBreak akishirikiana na Eddy Kenzo wa Uganda na Bisa Kidei wa nchini Ghana. Hii imepelekea mafanikio nchini mwake ikiwa ni miezi kadhaa video ya wimbo wa “Última Bolacha” ilizidi watazamaji Milioni 1 kwenye YouTube. Shellsy ameshinda tuzo ya Best Female Act na hii imefanya Coke Studio Africa imjumuishe kwenye list ya msimu wa mwaka 2019 akiwa kama msanii toka Mozambique. Mwaka huu, Shellsy atashirikiana na mkali Jux toka Tanzania.

THE JOURNEY

Shellsyy alikuwa sehemu ya kundi la tamaduni ambapo alikuwa mchezaji na mwanamitindo. Alihamasika kuendelea Zaidi kwenye muziki alipochaguliwa kwenye mashindano ya vijana na watoto nchini Marekani, ambapo alishinda nafasi ya pili. Baada ya mashindano kuisha alirudi nyumbani na kusainiwa na Game Over Entertainment ambapo aliachia ngoma ya Do not Break my heart. Na baadae aliachia albamu aliyoipa jina la Shellsy Baronet ambayo ilipokelewa vizuri na mashabiki. Katika Albamu hiyo aliachia nyimbo ya Ultima Bolacha. Kutoka hapo safari yake ya muziki ilizidi kupata mafanikio sana na pia kaweza kufanya shoo na wasanii mbalimbali kama vile C4Pedro na dada yake Zander Baronet. Shellsy ameweza kufanya shoo kwenye sherehe za Umoja wa mataifa kwenye sherehe za Siku ya ukimwi duniani na Tamasha la muziki wa Zouk.

SUPER WOMAN

Huku akiendelea kujipatia mashabiki,na kuwekeza jina lake kwenye tasnia hiyo amekuwa akihamasisha na kuwezesha wanawake na kuwasaidia shule mbalimbali nchini Mozambique, Hivi sasa yuko studio akirekodi nyimbo zake katika albamu yake ya kwanza ambayo anatarajia kuachia mwaka 2018 ambayo ameshirikiana na wasanii mbalimbali kutoka nchi za Lusophone na wasanii wengine mbalimbali.

SHELLSY’S STORY

Shellsy Baronet alizaliwa nchini Mozambique karibia maisha yake ya utotoni alikulia Afrika Kusini na Mozambique ambapo mapenzi yake kwenye muziki ndipo yalipogundulika. Safari yake ya muziki ilianza toka akiwa mdogo. Akiwa na umri wa miaka 10 akiwa anasoma nchini Afrika Kusini alijiunga na shule ya Sanaa ambapo ndipo alikuza muziki wake na vilevile alikuwa sehemu ya Dansi, Mitindo na Uigizaji. Wasanii wanaompa motisha ni Mingas, La Lizzy na Zander Baronet.