JUMA JUX

Akiwa na Nyimbo zilizokiki kama “Utaniua”, “Zaidi”, “Wivu” na “Juu” aliyomshirikisha Vanessa Mdee , Mtanzania Juma Jux ni staa wa  R&B mwenye staili na sauti ya kuvutia. Mwaka 2015, alinyakua tuzo ya Best R&B song kwenye Kili Music Awards (Tanzania). Kwa miaka mingi Jux amekuwa akishughulika na muziki na biashara kama CEO na mwanzilishi wa brand ya mavazi ya: African Boy. Muda huo huo, Jux pia alikuwa akiendelea na masomo yake China. Alidhamiria kulipa deni la mashabiki wake wa muziki ambao hawakumtupa. 2018 umekuwa mwaka mzuri kwake kwani amejihusisha na muziki kwa kiwango kikubwa. Atakuwepo kwenye Coke Studio Africa 2019 akishirikiana na mkali kutoka Zambia na Shellsy Baronet pembeni ya produza Lizer (Tanzania).

CAREER

Jux alianza kurusha karata yake ya muziki kwa wimbo, “Nimedata” mwaka 2005. Miaka mitatu baadae aliungana na Cyril Kamikaze na Gigga Flow kuunda kundi - Wakacha – ambalo lilidondosha ngoma kama “Facebook Gal”, “Here We Go” and “Mimi na Wewe”.  Tangu akifanya mzuki pekeyake, Jux amepiga makolabo na wakali wa Tanzania kama Joh Makini, Vanessa Mdee, Ben Pol, G Nako, Barakah Da Prince, na Navy Kenzo. Anafahamika kwa sauti yake nzuri, mafanikio yake ya muziki na amejipatia tuzo na kutajwa pia kwenye tuzo ikiwemo Best East African Music Video kwenye Zanzibar International Film Festival (2017), na wimbo wake wa “Umenikamata”.

 

MUSIC INTERESTS

 

Akiwa anapendwa kila mji Tanzania, Jux ni msanii mwenye hadhi ya juu. Mwaka 2018, akiwa na pop diva Vanessa Mdee, wapenzi hawa waliendesha shoo yao yenye mafanikio nchini Tanzania. Wamezunguka miji mitano ya Tanzania na kutumbuiza kwenye Tamasha walilolipa jina la “IN LOVE & MONEY TOUR”. Juma pia amefanya shoo mara kadhaa kwenye tamasha kubwa Tanzania la – FIESTA mwaka 2017, alijipanga na kufanya muziki na bendi katika tamasha kubwa la muziki ‘Love, Melodies & Lights’ akiwa na mastaa wengine wa R&B kama Ben Pol na Barakah da Prince.

 

BACKGROUND

 

Jina la kuzaliwa ni Juma Musa Mkambala mwaka 1989, Juma Jux amekuwa na wakati mzuri wa muziki wake hadi kufikia kuwa staa wa R&B . Tangu mwaka 2005, ameweza kuendelea kukiki kwenye muziki kwa ngoma baada ya ngoma. Juma anaendelea kujenga jina la brand yake ya nguo na muziki wake kwa kuachia albamu mwaka 2019.