RAYVANNY

VANNY BOY NI NANI?

Msanii kutoka Tanzania anaekua kwa haraka zaidi barani Afrika kwa sasa. Msanii pekee kutoka Afrika Mashariki aliyetajwa kwenye tuzo za BET mwaka huu 2017. Ni mshiriki wa International Viewer’s Choice Award- kuonyesha nguvu aliyonayo. Rayvanny anajulikana kwa ngoma zake kali kama vile ‘’Zezeta, Kwetu, Natafuta kiki na Salome aliyoshirikiana na Diamond Platnumz. Ndani ya coke studio 2017 Rayvanny atashirikiana na Dji Tafinha kutoka Angola.

KUTOKA KUWA MSANII MFUNGUZI HADI MSANII KABISA.

Rayvanny ameanza kung’aa kuanzia alipokua mfunguza wa shoo za msanii Madee akiwa chini ya uongozi wa TipTop Connection wakishirikiana na lebo ya muziki ya Mkubwa na Wanawe kwa miaka miwili, akaendelea kukuza muziki wake na kupata ujuzi wa kukuza kipaji chake zaidi. Kwa sasa amesainiwa chini ya lebo kubwa Afrika Mashariki ya Wasafi Classic (WCB) ambapo anazidi kukuza muziki wake huku akiachia ngoma moja baada ya nyingine. Rayvanny ameongeza namba ya shoo anazozifanya kama vile Serengeti Fiesta, Kilimanjaro Music Award na Safari za Kampeni za uraisi CCM mwaka 2015.

MAFANIKIO ZAIDI

Baada ya kuachia ngoma yake kali ya ‘’Kwetu” iliyofikia zaidi ya watu Millioni 7 kwenye mtandao wa Youtube imemjengea heshima na kuendelea kutambulika zaidi na wasanii wengine. Amesharikiana na wasanii wakubwa kama vile Diamond, Khaligraph Jones, Bahati na Queen Darleen, kama msanii wa Bongo Flava ameweza kukamata na kujiongezea zaidi mashabiki mjini kutokana na muziki wake unaokiki.

NYUMA YA MUZIKI.

Jina la kuzaliwa ni Raymond Shaban Mwakyusa mwaka 1993, Rayvanny alianza kupenda muziki toka alivyokuwa shule. Alishinda kwenye mashindano ya Freestyle ndani ya Serengeti Fiesta mkoani Mbeya mwaka 2011 na kuendelea kushinda mashindano mengi ya kitaifa zaidi yanayomuweka katika nafasi nzuri ya kimuziki. Hapo ndipo alitambulika na Tiptop Connection na kuamua kumchukua.