PATORANKING

KUTANA NA PANTORANKING.

Pantoranking ni msanii, mwandishi na muimbaji kutoka nchini Nigeria alieshinda tuzo nyingi, alijipatia umaarufu baada ya kutoa nyimbo yake ya Girlie O akimshirikisha mwanadada Tiwa Savage, Nyimbo zake zingine alizozitoa ni kama vile Daniella Whine,Alubarika na No Kissing baby akiwa na Sarkodie msanii kutoka Ghana.  Aina ya muziki anayotumia ni miondoko ya dance hall na Rege iliyomfanya awe tofauti na wasanii wengi katika soko la muziki. Alishiriki Coke Studio Afrika msimu wanne akishirikiana na mwanadada Vanessa Mdee. Amerudi kwenye shoo hii msimu huu mwaka 2017 akishirikiana na mwanamuziki Alikiba kutoka Tanzania.

KUPATA TUZO

Mwaka 2017, Pantoranking alishinda tuzo ya Msanii bora wa Afrika kwenye tuzo za muziki za nchini Afrika kusini zijulikanazo kama SAMA. Alichaguliwa 2015 kama msanii bora wa mwezi kwenye MTV Base, Patoranking alishinda tuzo ya msanii bora anaechipukia mwaka huohuo, pia alishinda tuzo ya msanii bora anaechipukia kwenye City People Entertainment Awards na tuzo ya Msanii anayetajwa sana kwenye tuzo za Sherehe za Headies mwaka 2014 nchini Nigeria. Mwaka 2014, alisaini rasmi dili la kurecord na lebo ya Foston Musik. Aliachia ngoma tano zilizotambulika. Baadhi ya sehemu alizofanya shoo ni kama vile Mauritus, New York, na tamasha la Notting Hill huko London akiwa na Msanii mahiri wa kimarekani Tinashe.

KUTOKA KWAKE

Patoranking alianza kung’ara kwenye muziki wa Naijeria kupitia style yake ya Dancehall, reggae na vionjo vya Kiafrika. Albamu yake ya kwanza iliitwa God Over Everything iliachiwa mwaka 2016. Nyimbo yake kali ya kwanza kuachiwa iliitwa Alubarika aliyoimba na Timaya mmoja kati ya Wasanii bora wa miondoko ya dancehall. Nyimbo hiyo ilikua na maana Baraka za Mungu ambayo ni stori yake ya kweli kutoka alipotoka na alipo sasa.

 STORI YA MAISHA YAKE

Patoranking, ni mtoto wa mwisho kati ya watoto watano katika familia yake, amekulia kwenye mji mdogo wa Ilaje ndani ya Lagos nchini Nigeria. Aliishi maisha ya kimaskini yeye na familia yake iliyopelekea awe mzururaji mitaani katika umri mdogo. Hiyo ilimpelekea yeye aanze safari yake ya kimuziki ili aweze kuishi maisha mazuri yeye na familia yake. Kazi yake ilianza kuonyesha matunda pale alipoanza kufanya kazi ya pazia na wasanii kama XProject, Konga, Slam na Reggie Rockstone.