NYASHINSKI

KUTANA NA MFALME ANAYERUDI.

Nyashinski ni msanii wa Kenya anajulikana zaidi kama mfalme anayerudi kwa kasi, hivi karibuni aliachia ngoma mbili kali Aminia na Malaika. Nyimbo zake zingine alizoachia hivi karibuni ni kama vile Letigo aliyomshirikisha Nameless, now you Know na Mungu Pekee. Mwaka 2016, Nyashinski aliingia ndani ya Coke Studio huku akiungana na Yemi Alade kutoka Nigeria na Rubi msanii anayechipukia kutoka Uganda. Katika msimu huo pia alikuwa ni mmoja kati ya wasanii mbalimbali barani waliyoweza kushirikiana na msanii mahiri kutoka marekani Trey Songz. Amerudi ndani ya Coke Studio 2017 akishirikiana na kundi maarufu la wasanii kutoka Afrika Kusini lijulikanalo kama Mafikizolo.

KURUDI KWAKE.

Safari ya muziki ya Nyashinski ilianza alivyokuwa na kundi maarufu la muziki nchini Kenya lililokua likifahamika kama Kleptomaniax. Baada ya kundi kuvunjika, Nyashinski alihamia nchini Marekani na baada ya miaka kadhaa alirudi nchini Kenya na kuachia nyimbo yake ya kwanza ya Letigo aliyomshirikisha Nameless na kumfanya aweze kujulikana. Mwezi wa tano mwaka 2016, Nyashinski aliachia nyimbo yake ya kwanza ya miondoko ya solo na video ijulikanayo kama Now You Know, iliyofanya itazamwe mara milioni moja kwenye mtandao maarufu wa Youtube miezi sita(6) baadae ilikua ndio video ya kwanza ya msanii rapa nchini Kenya kupata watazamaji wengi. Nyimbo yake ya Mungu Pekee aliyoiachia Oktoba mwaka 2016 ilisikilizwa zaidi Kenya na Mataifa mbalimbali.

NAMBA MOJA

Nyanshiski ameendelea kufanya shoo katika sherehe na Matamasha mbalimbali Afrika Mashariki na kufanya muziki wake uweze kushika chati zaidi. Mwaka 2016 alishinda Tuzo ya miziki ya video ya Pulse kama Video bora ya msanii wa kiume iliyotazamwa zaidi mwaka huo.

NYUMA YA MUZIKI

Jina lake halisi anajulikana kama Nyamari Ongegu, Rapa huyo alizaliwa mwaka 1984 na kuibukia kutoka kwenye kundi la muziki la Kleptomaniax,Ambapo walikutana kipindi wapo Sekondari mjini Nairobi.