MAFIKIZOLO

MAFIKIZOLO NI KINA NANI?

Ni kundi la wasanii kutoka nchini Afrika Kusini lililojipatia heshima kama kundi la muda mrefu barani Afrika. Wanajulikana kwa nyimbo zao za miondoko ya Afro-Pop,Kwaito,Kwela na Marabi, Mafikizolo waliiteka bara la Afrika kwa nyimbo zao zilizotamba kama vile Ndihamba Nawe na Khona. Washindi wa Kundi bora la mwaka kwenye tuzo za MAMAs mwaka 2014 na pia wameshinda mara tatu(3) kwenye tuzo za muziki nchini Afrika Kusini zijulikanazo kama SAMA kna tuzo ya Kundi bora la mwaka. Kundi hilo waliingia kwa mara ya kwanza ndani ya Coke Studio wakishirikiana na mwanamuziki Nyashinski kutoka Kenya.

Kundi hilo lilianza mwaka 1996, walianza na nyimbo za miondoko ya Kwaito iliyofanya wapate dili la kurekodi kwenye studio za Kalawa Jazmee Records. Walitengeneza Albamu mbalimbali kama vile Mafikizolo ya mwaka 1999, Gate Crashers(2000) na Kweka mwaka 2003 kabla ya kuanza mapumziko ya muziki. Walirudi kwenye soko la muziki na kuachia Albamu yao ya saba iitwayo Six Mabone lengo likiwa ni kuwarudisha mashabiki zao ndani ya safari yao ya muziki rekodi hiyo ilihusisha uwepo wa nyimbo ya Walila ya mwanamama Miriam Makeba na Flowers aliyomshirikisha Zonke. Albamu yao ya nane iliitwa Reunion ambayo ilikua na ngoma ya Khona iliyorudisha Umaarufu wao kwenye soko la muziki huku wakimshirikisha Uhuru. Na nyimbo mbalimbali kama vile Chalete waliyomshirikisha Davido na May D waliyomshirikisha Happiness.

Ndani ya Coke studio walitangaza kuwa wanategemea kuachia albamu yenye nyimbo 20 kama zawadi kwa mashabiki zao ikiwa wanatimiza miaka 20 toka waanze safari yao ya muziki.

MWANZO

Mafikizolo lilikua kundi la muziki wa kwaito lakini walibadili muziki wao kwenda miondoko ya Afro-Pop. Kgosinkwe wa mafikizolo anasema “hatutengenezi albamu kwa ajili ya mwisho wa mwaka bali kwa muziki utakaodumu milele”.

Wanaendelea kujipatia mashabiki kila kona ya bara la Afrika huku wakishirikiana na wasanii kama vile Diamond na Jaguar na nyimbo yao ya Kiswahili iitwayo Kucheza.

AINA YA MUZIKI

Ukimtaja Theo Kgosinkwe na Nhlanhla Nciza, kundi hilo lilianzishwa na Kalawa Jazmee mwaka 1996, Katika majaribu waliyopata kundi hilo ni mwaka 2004 walipompoteza mwanakundi mwenzao Tebogo Madingoane mwaka 2004 huko Tebza. Baada ya muda mfupi kujulikana Walihusishwa kwenye ajali iliyopelekea baadhi ya wanakundi kukaa hospitali kwa wiki kadhaa.Kundi hilo limekutana na majaribu mbalimbali hadi kusimama kama kundi mahiri barani Afrika.