IZZO BIZZNESS

IZZO NI NANI?

Msanii wa Hip-hop aliyeibukia kutoka nchini Tanzania Izzo business ni msanii anaefahamika Afrika Mashariki na nyimbo zake zilizojipatia umaarufu kama Umeniweza na Tumeoana aliyoshirikiana na abela Music. Mwaka huu ndani ya Coke Studio Izzo business ameingia akiungana na Mwanadada avril kutoka Kenya aliyerudi kwenye shoo hii kwa mara ya pili sasa.

SAFARI YAKE.

Izzo Business alirecord nyimbo yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 18 na alijiunga rasmi na kua chini ya lebo ya MJ RECORDS mwaka 2010. Hapo ndipo safari yake ilipoanzia na kumfanya aanze kufahamika ndipo alipoachia wimbo wa Business aliyomshirikisha Sumalee na Tenzi za mapenzi aliyomshirikisha Shapsin. Amewahi kushiriki kwenye za Kilimanjaro Music awards na mwaka 2013 alitajwa kuwania Tuzo za watu. Pia ameshirikiana na msanii kutoka Uganda Navio, na pia mtayarisha muziki Fundi Samweli kutoka Sweden, vilevile Mwasiti, Dully Sykes, Ben Pol, AY na wengine wengi.

NINI CHA TOFAUTI KWENYE MASHAIRI YA IZZO?

Sanaa ya Izzo inalenga zaidi maisha kwa jinsi anavyoyaona akichanganya na Hisia ,lugha ya picha, na ukweli halisi. Msanii huyu amepata bahati ya kushiriki jukwaa moja na msaani anaeheshimika kutoka nchini Marekani Ludacris na Busta Rhymes.

WAPI ALIANZIA?

Emmanuel Simwinga maarufu kama Izzo business alizaliwa mkoani Shinyanga na kukulia mkoani Mbeya lakini kwasasa makazi yake maalumu ni Dar es Salaam. Ana Astashada ya masoko na uongozi kutoka chuo cha biashara CBE, pia mbali na muziki ni mjasiriamali asiyependa kuweka mambo yake ya biashara na uwekezaji hadharani.