EDDY KENZO

EDDO KENZO NI NANI?

Eddy ni kenzo ni aina ya mwanamuziki ambaye hupendelea kuvaa mavazi ya aina yake ili kuonyesha maisha ya kawaida ya Uganda. Mapenzi yake kwa muziki na kucheza mara nyingi huonekana ndani ya video zake. Alikuwa ndiye sababu ya video ya Sitya Loss iliyotazamwa zaidi Afrika Mashariki ambayo pia iliunda kundi la vijana la muziki lililojulikana kama kama Ghetto Kids. Ikitangaza aina ya muziki kwa miondoko ya Afro beat na Dancehall ambayo inamfanya aendelee kusimama imara. Baadhi ya ngoma zake kali ni kama vile Stamina na Yanimba. Ndani ya Coke Studio 2017 Eddy ameingia huku akishirikiana na mwanamuziki Bisa Kdei kutoka Ghana.

KUTAMBULIKA KIMATAIFA

Kufuatia tuzo yake ya BET aliyoshinda mwaka 2015 ya Msanii Bora Wa Kimataifa Anayechipukia, Kenzo alienda kwenye tuzo kadhaa za kimataifa  ikiwemo Msanii bora wa Afrika kwenye Tuzo za Muziki za Nigeria mwaka 2015, Video Bora ya Muziki 2015  kwenye Tuzo za Muziki nchini Uganda, Msanii bora anayetumia Mitandao ya Kijamii kwenye Tuzo za muziki za Hipipo mwaka 2015 na Video bora ya mwaka kwenye tuzo za African Entertainment mwaka 2015 nchini Marekani na zinginezo. Kenzo amefanya shoo sehemu mbalimbali duniani ikiwemo kwenye sherehe za SXSW Austin, Texas mwaka 2015 na kwenye Ligi ya mataifa ya Afrika huko Equatorial Guinea, Gabon,Ivory Coast, UK na Cameroon.

KUTUSUA KWAKE

Eddy Kenzo alivunja rekodi nchini Uganda kwa mara ya kwanza kwenye sherehe za muziki za Uganda mwaka 2008 na nyimbo yake ya Yanimba.  Ikifuatia na nyimbo yake ya Stamina iliyojipatia pia mafanikio. Eddy alitambulika zaidi mwaka 2014 alipoachia wimbo wa Sitya Loss uliyopelekea kutazamwa na zaidi ya watu 100,000 kwa siku ambayo pia wasanii mbalimbali waliweza kuisikiliza kama vile Ellen Degeneres, P.Diddy, Akon,Ronadinho,Tevin Campbell, na Sanaa Lathan.

NYUMA YA MUZIKI.

Eddy Kenzo ni mkazi halisi wa eneo la Mji wa Masaka nchini Uganda, akiwa na miaka minne Eddy alimpoteza mama yake ambapo alilazimika kuishi kama mtoto wa mtaani kwa miaka zaidi ya 13. Muziki ndiyo uliomfanya atoke huko alipokuwepo na kuwa alipo sasa.