DENISE

DENISE NI NANI?

Mkali wa sauti kutoka Madagascar, Denise ni msanii kutoka Afrika wa kumuangalia. Kwasasa anatamba na wimbo wake wa Allofo, anaibuka kwenye Coke Studio Africa mwaka 2017 akikiwasha stejini pamoja na rapa Nasty C kutoka Afrika Kusini na Mnaijeria Runtown zote zikiwa zimetayarishwa na produza Shado Chris kutoka Ivory Coast.

ALIVYOTOKA

Denise ameanza kutambulika mwaka 2014 aliposhinda sehemu ya kwanza ya shindano la Pan Africa la Island Africa Talent.  Alikuwa na kipenzi cha mashabiki tangu mwanzo, ushindi wake ulimpa nafasi ya kurekodi Universal Music. Ngoma yake ya kwanza ya Allofo ilifanyika Lagos, Nigeria na tayari imepata kuchezwa mara nyingi barani. Akisaidiwa na producer Kimfu, High P, Black Kent, 2B na Thomas Azier, pia mkali huyu anafanya kazi na mume wake Shyn ambaye ni mwandishi na mtengenezaji muziki. Denise kwa sasa anafanyia kazi albamu yake ya kwanza ambayo amepanga kuonyesha thamani na ukweli.

MOTISHA

Denise alivutiwa na stori za zama za kale za jamii anayotokea na pia kuvutiwa na baadhi ya mataifa mengine. Mapenzi yake kwa mabadiliko ya utamaduni yameendelea kuukuza muziki wake. Denise pia ni mtengeneza picha za video, na kwa sasa anashirikiana na mbunifu Pierre-Christophe Gam kuitangaza Africa, ambapo wamedhamiria kuonesha utofauti miongoni mwa vijana wa Africa.

MBALI NA MUZIKI

Mwanamuziki huyu mwenye miaka 28 ameishi nusu ya miaka yake jukwaani, sehemu pekee aipendayo. Katika umri mdogo alivutiwa na stori za familia yake, alitumia muda wake wote kuandika nyimbo na kushinda studio. Amerithi kwa babu yake aliyefahamika kwa kipaji chake. Ndooto ya Denise kusafiri duniani na kuwa ndani ya mioyo ya watu.