Dawit Nega

Ukipata nafasi ya kusikiliza muziki wa Ethiopia moja kwa moja utaelewa kwanini mkali Dawit Nega ametusua. Akiwa na ngoma zaidi ya tano zikiwa na jina lake, video zake zimepata watazamaji zaidi ya laki moja kupitia YouTube. Kwenye msimu huu wa Coke Studio Africa, Dawit ni Big Break Artist, akifanya yake na Muangola Ansellmo Ralph na nyota maarufu Mi Casa toka Afrika Kusini.

SAFARI YA MUZIKI

Safari ya muziki ya Dawit ilianza miaka kadhaa iliyopita na video zake zilizokuwa Youtube mwaka 2013. Hana albam yoyote, lakini ana nyimbo kama Deamena, Kem Gelgele Meskel, Baba Elen, Wezamey na Ziwedero zilizompatia umaarufu nchi nzima. Wezamey iliachiwa mwaka 2016 na imepata zaidi ya watazamaji million 8 na ilipigwa live na Dawit kwenye tamasha la Melbourne nchini Australia.

KUPATA UMAARUFU

Kilichompa Dawit umaarufu ni mapenzi yake ya kueneza utamaduni wa Ethiopia kwa vijana na wimbo wake wa Tigrigna. Tigrigna lafudhi tofauti kutoka wazungumzaji wa lugha ya Amharic nchini Ethiopia. Lengo Dawit Nega ni kueneza utamaduni wa Tigrigna duniani

MBALI NA MUZIKI

Dawit Nega alizaliwa na kulelewa Mekelle, Ethiopia. Ana Imani kubwa kwamba vijana wana nafasi kubwa sana kwenye kueneza utamaduni wa Ethiopia na kutumia nafasi hiyo kupitia muziki wake.