CHIDINMA KATIKA SAFARI YAKE YA MUZIKI

Mwanamuziki mashuhuri nchini Nigeria ajulikanae kama Chidinma aka Miss Kedike, amerudi tena kwenye coke studio Afrika kwa mara ya nne mwaka huu akishirikiana na wasanii mahiri kutoka Kenya wanounda kundi la Sauti Sol. Nyuma ya studio hizi kwenye shoo Mwanadada Chidinma ameshea nasi stori yake kuhusu safari yake ya muziki toka alipoanza.

Kutokea Umri mdogo – alikua akipenda muziki.

Akiwa mototo, Chidinma Ekile alifanya kila awezavyo kufata ndoto zake. Katika kumbukumbu zake aliwahi kulala nje kwasababu ya mapenzi yake kwa muziki. Anasema “Sikufanya vitu vingi nilipokuwa mdogo kwasababu nilikua na baba Mkali”. Kuna siku nilisikia kuhusu mashindano ya kwaya niliamua kwenda kujaribu, nilipitiliza muda na kufanya nichelewe kurudi nyumbani, nilikua na kaka yangu mdogo kwahiyo nikajua baba atakubali tuchelewe, lakini tulivorudi nyumbani kaka yangu mdogo akaruhusiwa kuingia ndani mimi sikuruhusiwa kuingia nikajua utani lakini haikuwa hivyo nikalala nje huo usiku.

Asingekua msanii Chidinma angekuwa Mtangazaji

Chidinma anasema mafanikio yake alianza kuyaona mapema katika safari yake ya muziki baada tu ya kutoa wimbo wake wa kwanza wa Kedike, kitu ambacho caught her off guard. Anasema alishangazwa na jinsi wimbo wake livyokua kwa haraka ndani ya bara la Afrika kwa muda mfupi na hiyo ikamfanya aweze kusimama imara. Chidinma anaongeza kama isingetokea hivo basi angekua mtangazaji “Nilikua nikipenda kusoma magazeti kwa sauti kubwa huku nikijitazama mbele (kwenye) kioo”. Lakini wimbi la muziki lilipoibuka akaamua kukimbilia huko.

Sipendi Uongo – Anasema Chidnma

Chidinma anajulikana kwa kuwa hodari na mchapakazi. Kitu gani kinampeleka mbio? “Siwezi kusimamia uongo”. Binti Kedike atakua rahisi kukuondoa katika maisha yake akigundua kama umemdanganya. Anasema “labda ndio sababu sina marafiki wengi”. Kwa upande mwingine, Chidinma anasema alichaguliwa katika mashindano yaliyomletea matatizo kwa baba yake akiwa mdogo, mengine ni historia kama wanavyosema.