BUSISWA

BUSISWA NI NANI?

Malkia wa dance wa Afrika kusini anarudi mara ya pili kwenye Coke Studio Africa mwaka 2017 akishirikiana na rapa Slapdee kutoka Zambia.

Mwanadada huyu mwenye kipaji ambaye sauti yake imetengeneza nyimbo kama Lahla na Ngoku hawezi kuacha kutajwa bila ngoma yake iliyotisha sana ya My Name Is ambayo ilifanya wimbo wa DJ Zinhle kufanya vizuri.

Akiongea na Coke Studio nyuma ya studio za Coke Studio mjini Nairobi, Busiswa amesema: “Coke Studio inafanya kazi kubwa sana lakini pia ni moja ya vitu vinavyovutia sana ambavyo sikuwahi kufanya. Inasisimua! Kila siku ni tofauti. Unakutana na watu wapya na kupata changamoto mpya”

MTUSUO

Busiswa alianza kufanyia kazi kipaji chake kwa kuchanganya maneno na muziki wa dansi mwaka 2010 ambayo ilimpatia nafasi ya kurekodi na mtayarishaji wa muziki wa house Sir Bubzi na DJ Clap. Amepanda jukwaa moja na wakali kama Mak Manaka, Lebo Mashile na Gcina Mhliphe. Safari yake ya mafanikio ya muziki imempa ushindi wa Mtumbuizaji Bora kupitia wimbo wa Ngoku alioshirikiana na Oskido na Uhuru kwenye tuzo za Chanel O, pia ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike ya Afrimma (2015) na Mwanamuziki Bora wa Kike kupitia tuzo za Mzanzi Kwaito (2016). Pia alitajwa kama mmoja wa vijana hodari 200 wa south Africa na Mail and Guardian (2014), tuzo za Metro FM (2015), Mkutano wa Winter Music (2015), Bang the Drums UK tour (2015), Big Brother Africa na Idols SA.

ALIPOTAMBULIKA DUNIANI KOTE.

Wimbo wake uliofanya vizuri wa Lahla ulitumika kama sehemu ya soundtrack ya filamu ya Honey 3: Dare to Dance. Filamu hii ilikuza jina lake na kuanza kuzungumziwa duniani kote pamoja na muziki wa dansi wa Afrika Kusini.

HISTORIA

Akiwa mzaliwa wa Cape Town, mjini Umtata, Busiswa Gqulu aliishi Maisha yake akiwa chini ya uangalizi wa marehemu mama yake na bibi yake, ambao walikuwa wakimuongoza na kumtengeneza kufikia kuwa alivyo. Kusoma na kuandika mashairi ndicho kitu alichopendelea katika umri mdogo, ambapo alianza kushiriki kwenye matamasha akiwa na miaka 10. Kikubwa zaidi, alitajwa kwenye tamasha kubwa na ushairi la Poetry Africa International Festival mara mbili, akiwa na wanamshairi wengine duniani