BRUCE MELODIE

WHO IS MR. MEODIE ?

Rwanda inaingia kwenye Coke Studio Africa mwaka huu kupitia mwanamuziki wa R&B Bruce Melodie, anayefahamika kwa ngoma kama “Ndumiwe” na “Incwi”. Bruce amekuwa akishirikiana na wasanii maarufu kama Khaligraph Jones anayetamba na style yake ya kuchana kwa kasi na ngoma kama “Micasa Sucasa”. Bruce atashirikiana na producer Dj Maphorisa wa South Africa.

Bruce ni mshiriki wa tuzo za muziki za Hipipo za Uganda akiwania wimbo wa mwaka (Rwanda) kupitia “Turabeeranye”. Pia ni mshindi wa tuzo ya msanii bora wa R&B wa mwaka mara mbili mfululizo wa tuzo ya Salax (2013, 2014).

MR. INDEPENDENT

Baadhi ya vitu vinavyofanya Bruce Melodie awe mkali ni kipaji chake na kubadilika. Muimbaji huyo pia ni mpgigaji na mtayarishaji wa muziki. Album yake “Ndumiwe” iliachiwa Agosti 2013 wakati akiwa chini ya The Super Level – lebo kubwa ya muziki Rwanda. Iliyompeleka kwenye umaarufu, albamu iliyokuwa na ngoma kama “Ndumiwe”, “Tubivemo” na “Incwi” ikishirikisha wasanii wa Uganda Jamal na “Music” na Radio wa Uganda Radio & Weasel. Albam ya pili ya Melodie “Ntundize” iliachiwa mwaka 2014 ikifuatiwa na mafanikio ya album yake yenye mkusanyiko wa nyimbo kali kama “Ntundize” and “Ntujya Unkinisha” zilizofanya vizuri sokoni.

MWANZO WA SAFARI

Bruce Melodie alianza kutengeneza kipaji chake cha sauti akiwa na umri mdogo, akiimba kwaya kanisani. Hii ilimpa motisha wa kuwa mtayarishaji wa muziki. Baadae Bruce alikuja kuwa msaidizi wa wasanii kadhaa Rwanda. Akipewa motisha na mafanikio ya kundi la muziki kama Kigali Boys na Family Squad, Bruce aliamua kuendelea safari yake ya muziki.

HISTORIA

Alizaliwa kijiji cha Kanombe, kata ya Kicukiro mjini Kigali na baba mwanajeshi na mama mfanyabiashara mdogo kijijini, Bruce ana ndugu watatu.

Alisoma shule ya msingi ya Camp Konombe kabla ya kumaliza masomo ya shule ya Sekondari Rwamagana Islamic. Ameoa na ana mtoto wa kike, Itahiwacu Britta aliyezaliwa mwaka 2015. Mbali na muziki Bruce anapenda kuigiza, na amewahi kushiriki kwenye moja ya tamthilia ya “Seburikoko”