ANSELMO

KUTANA NA ANSELMO

Mkali Anselmo Ralph kutoka Angola ni nguli aliyehai. Safari yake ya muziki imezidi muongo mmoja sasa, anaendelea kupata mafanikio kila albam mpya anayotoa. Mkali huyu ametengeneza muziki wa kimataifa na muziki wake umepokelewa vizuri nje Angola. Amejishindia Tuzo ya muziki ya MTV kipengele cha best Lusophone. Mwaka huu atakuwepo kwenye Coke Studo Africa akipiga shoo matata na Mi Casa.

HISTORIA YA MAFANIKIO YA NGULI HUYU

Moja kati ya wasanii wenye mafanikio nchini Angola, Anselmo ana albumu kibao. Albamu yake ya “Stories of Love” (2006) imemuweka kwenye ramani na kumtambulisha kwa mashabiki. Mwaka huo huo, alitajwa kama msanii bora wa RnB na kituo cha Televisheni cha South Africa vile vile kama Msanii bora Africa na tuzo za MTV Europe. Ameendelea na kuachia "The Last Stories of Love" (2007), "O Cupido" (2009), "A Dor Do Cupido"(2013), "O Melhor de Anselmo Ralph" (2014) and "Amor É Cego" (2016). Anathamiwa sana nchini Angola na amekuwa mwalimu wa The Voice, Angola tangu 2014. Juni 2015, Anselmo amesaini mkataba na Sony Music Entertainment Spain ambayo imeupeleka muziki wake kimataifa zaidi.

MATAMASHA DUNIANI KOTE

Albam yake ya mwisho imekuja na njia mpya na kupanua mipaka zaidi kwenye soko la muziki la Africa kwa kuvutia watu na kuleta aina mpya kwa mashabiki. Anselmo amezunguka kufanya matamasha Portugal, Holland, England, Mozambique, South Africa, Sao Tome na Principe, Brazil na Namibia.

MBALI NA MUZIKI

Anselmo Ralph alizaliwa mwaka 1981 nchini Luanda ambapo alihudhuria shule. Baada ya kuishi kwa miaka kadhaa jijini Madrid, mapenzi yake kwa muziki yaliongezeka na alikuwa shabiki mkubwa wa Juan Luis Guerra. Alihamia New York ambapo alifanya masomo yake Borough ya Manhattan Community College. Hapa ndipo alipojiunga na band ya Rock ‘n’ roll kabla ya kurudi nyumbani. Anselmo ameweka nguvu kwenye mikakati yake kama NGB (New Generation Band) nchini Angola ambayo alirekodi nayo albamu yake ya kwanza kabla ya kufanya kazi kivyake. Ameendelea kufanya vizuri na sasa ameweka nguvu kwenye kupata soko la Amerika Kusini, Ulaya na Afrika nzima.