AMANDA BLACK

Amanda Black ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo na mpiga gita kutoka South Africa ambaye ameweza kufahamika mwaka 2016 baada ya wimbo wake ulifanya vizuri wa Amazulu, ambao umefika platinum ndani ya wiki tatu tangu uachiwe. Wimbo ulishika chati kwa wiki 10 na kufanya kuwa moja ya wasanii waliouza kwa wingi kutoka South Africa 2017. Mkali huyu mwenye vipaji vingi ataungana na Joey B kwenye Coke Studio Africa 2017.

ALBAM YAKE

Amanda Black alianzia kwenye South African Idols mwaka 2015, ambapo alifika mpaka kwenye nyimbo 10 bora. Amanda alihamia Johannersburg Januari 2016 kuendelea na safari yake ya muziki, na kusainiwa na lebo ya kurekodi ya Ambitiouz Entertainment. Julai 1 mwaka huo, Amanda aliachia wimbo wake wa kwanza uiotwao Amazulu kutoka kwenye album yake ambayo ilipokelewa vizuri. Mwezi mmoja baada ya kuichia, album iliuza zaidi ya nakala 31,000 na kufika platinum.

#AMANDABLACKNIMSHINDI

Mwaka 2017 kupitia tuzo za muziki za Metro FM, alichaguliwa kama mshiriki kuwania vipengele 5 na kushinda Best R&B na tuzo ya chaguo la wasikilizaji. Pia amejishindia tuzo 4 za South African Music Awards za Album Bora ya Mwaka, Msanii mpya wa Mwaka, Msanii bora wa kike wa Mwaka na Album bora ya R&B Soul Reggae.  Ameng’aa kwenye matamasha makubwa ya South Africa kama Tuzo za 11 za Filamu na TV za mwaka nchini South Africa, Tuzo za 16 za Muziki Metro FM na Tamasha la wazi la Durban Jazz. Shoo yake ya kibabe ilifanya atajwe kama msanii wa kumtazama mwaka 2017 na MTV Base.

NJE YA MUZIKI WA AMANDA BLACK

Jina la kuzaliwa ni Amanda Benedicta Antony mwaka 1993 mjini Mthatha, Mashariki ya Cape Town, South Africa. Mapenzi yake kwa muziki yalianzia kanisani akiawa na umri mdogo na kupata mwaliko wa kuimba kwenye matamasha ya familia. Baada ya kumaliza shule aliendelea na elimu Nelson Mandela Metropolitan University, alipohitimu Diploma ya Elimu ya Muziki. Ametokea kwenye matoleo matatu ya South African Idols na kujitambulisha mwenyewe kama moja kati ya wasanii wenye ushawishi South Africa.