ALIKIBA

KUTANA NA MFALME KIBA

Mwandishi na muimbaji maarufu kutoka Tanzania Alikiba au maarufu zaidi kama King Kiba Amezidi kufahamika zaidi baada ya kusaini na lebo ya muziki ya Sony,amepewa zaidi heshima na mashabiki wake kutoka ndani na nje ya nchi kwa kumpa nguvu ya kutosha, Miaka ya hivi karibuni Alikiba amepokea tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya msanii bora wa Afrika kutoka MTV  Europe Music pamoja na The sound City MVP Awards kutoka nchini Nigeria na tuzo ya Chaguo la watu maarufu kama People Choice Award kama Msanii bora wa kiume wa Mwaka zote hizi mwaka ni 2016. Pia ni msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwekwa kwenye list ya Global Hip-hop inayomilikiwa na jarida la THE SOURSE huffington. Alikiba Amerudi kwa mara ya pili ndani ya Cokestudio 2017 huku akishirikiana na msanii Pantoranking kutoka Nigeria.

Inapokuja kwenye kuchezwa radioni na chati ya mauzo ripoti inaonyesha hana mpinzani kwa miaka iliyopita. Kila wimbo aliotoa tangu alipoanza muziki umekua ukishika namba 1 kwenye chati, Nyimbo ya Mwana inahesabiwa kama nyimbo kali zaidi na ilivunja rekodi kwenye Mkito kama nyimbo iliyopakuliwa zaidi.

PALE MOTISHA INAPOKUTANA NA UPENZI WA MUZIKI

Alikiba anamtaja Usher Raymond kama mtu anaempa motisha katika kazi zake. Mfalme huyu anafamika zaidi kwa kuteka Jukwaa la moja kwa moja, katika shughuli na matamasha mbalimbali. Amezunguka na shoo ya Fiesta kwenye mikoa zaidi ya 6 na pia kwenye tamasha la Koroga nchini Kenya. Mbali na muziki Alikiba anavutiwa zaidi na mazingira mwaka 2015 alichaguliwa kama mmoja wa mabalozi wa WILDAID’s Global Ambassadors kwenye kampeni ya Kuokoa Tembo akiungana na Wasanii na watu Mashuhuri duniani kama vile Lupita Nyong’o, David Beckam, Leonardo Dicaprio, Sir Richard Branson, Jackie Chan, Prince William of the United Kingdom, Fergie from the Black Eyed Peas. Wote walihudhuria kwenye uchangishaji pesa huko Bevery Hills katika mji wa Los Angeles nchini Marekani na kufanikiwa kupata zaidi ya Dola Milioni 5 kwa lengo hilo. Alikiba pia amethibitisha kuungana na Mpishi Maarufu Kutoka Uingereza Jamie Oliver kama Balozi wa ‘Champion for Food Revolution’ nchini Tanzania.

ALIANZA VIPI

Baada ya kumaliza shule mwaka 2004, Alikiba aliandika nyimbo yake ya kwanza ya Maria na kuendelea kutoa ngoma baada ya ngoma. Baadhi ya nyimbo ni kama vile Najuwa, Ndugu wangu, Kuteseka, Namshukuru Mungu, Sabrina, Yatima. Albamu zake ni pamoja na Cinderella (2008) na Ali K for Real (2009). Ametangaza kutoa albamu nyingine mpya mwisho wa mwaka 2017.

Raisi mstaafu Jakaya Kikwete alimempongeza Alikiba kwa kuchangia na kutangaza vyema Muziki, sanaa na utamaduni wa Tanzania. Alikiba pia ameweka historia kama msanii wa kwanza kutoka Afrika mashariki kufanya tour Tanzania nzima. Safari iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa iliyomzungusha mikoa yote Tanzania na kupiga shoo za nguvu zilizoweza kujaza nyomi kila ukumbi.