AKA

SUPAMEGA NI NANI?

Ni mshindi wa tuzo, msanii wa hiphop na producer AKA kutoka South Africa ni kipaji kisicho na shaka na rapa wa kuaminika. Anajulikana pia kama “Supa Mega”, AKA kwa sasa anatamba na ngoma yake ya The World Is Yours na Caiphus Song na Caiphus Song pamoja na nyimbo za kushirikiana kama 10 Fingers na Don’t Forget to Pray na mkali Anatii. AKA atakiwasha kwenye Coke Studio Africa mwaka huu akishirikiana na mnijeria Olamide.

SAFARI

AKA alianza kung’aa mwaka 2009, baada ya kuwa na ngoma kama Mistakes in My Walk na Do It, ambazo ziliingia kwenye chati za nyimbo bora 40 za South African 5M. Tangu hapo AKA amekuwa akifanya vizuri na nyimbo na albam ambazo zimefika kwenye chati za Afrika na Ulaya. AKA amefanya kazi na wasanii kibao kama Burna Boy, Diamond, Ice Prince, Khuli Chana, Yanga, Anatii, na KO. Mbali na muziki , pia ni mtayarishaji wa kipindi cha TV cha Hustle, ambacho kinaibua marapa wanaochipukia kuingia kwenye soko la muziki wa South Africa na kujipatia dili la kurekodi.

LEVELS KWENY MUZIKI

Rapa huyu mwenye miaka 29 amejinyakulia na kushiriki kwenye tuzo mbali mbali duniani. Ikiwemo album namba moja kwenye Itunes South Africa, wimbo bora wa kushirikiana wa Run Jozi alioshirikiana na KO, Video bora ya mwaka kupitia Congratulate, nyimbo mbili zilizofikia mauzo ya Gold, wimbo bora wa Metro FM na wimbo bora wa kushirikana “Baddest” na album ya “Levels” iliyofika Platinum. AKA pia ni mshiriki wa Tuzo ya BET kama msanii bora wa kimataifa – Africa. Ameendelea kutengeneza jina lake ambalo limempatia biashara, kuendesha shughuli mbalimbali na matamsha tofauti duniani.

ILIPOANZIA.

Jina halisi Kiernan Jarryd Forbes, AKA alizaliwa Cape Town, South Africa. Kutoka kushika chati hadi kushinda tuzo, mkali huyu amjijengea jina kama msanii anayetazamwa na bara zima pale anapotoa ngoma mpya.s to winning awards, the young musician has built a name for himself as a man whom the continent stops to listen to when he drops a new jam.