VANESSA MDEE

NCHI ALIYOTOKEA : TANZANIA
AINA YA MUZIKI : RNB, AFRO POP, HIP-HOP

KURASA ZA KIJAMII

   

VANESSA MDEE

Vanessa Mdee ni msanii wa kike anayeheshimika Afrika mashariki. Ni malkia wa miondoko ya POP Afrika mashariki na kipenzi cha Watanzania. Alishirikiana na 2Baba kutoka Nigeria katika msimu wa 3 wa Coke Studio Africa. Katika kipindi cha matayarisho ya album yake ya “Money Mondays” Vee anarudi Coke Studio msimu wa 4 akishirikiana Patoranking, msanii wa Nigeria.

KAZI

Baada ya kifo cha ghafla cha baba yake aliamua kufuata ndoto zake na kushiriki katika mashindano ya kumtafuta MTV Base VJ na kuibuka kuwa Mtanzania wa kwanza kuwa MTV VJ. Kabla ya kuamua kutulia katika kazi yake ya muziki, Vanessa alikuwa mtangazaji wa radio, TV na katika dhifa mbalimbali. Katika utangazaji ameshakutana na wasanii mbalimbali wa kimataifa kama vile French Montana na Jay Z.

MASLAHI NA MUZIKI

Akifurahia mafanikio ya nyimbo zake na video ambazo zimeenea kila mahali, Vanessa pia anajivunia kuwa miongoni mwa wanamuziki wenye mashabiki wengi mtandaoni Afrika. Bado anaendelea kufanya ziara na kusafiri sana kwa kufanya maonyesho na wachezaji wake wa kike. Ni mwanamke mwenye nguvu katika kazi yake na anayeng’ara ipasavyo. Akishirikiana na mtayarishaji mashuhuri wa muziki Tanzania, Nahreel. Kati ya nyimbo zake zinazovuma ni Hawajui, Siri, Nobody but Me and Niroge.

HISTORIA

Vanessa Hau Mdee, msichana mahiri Afrika Mashariki anayetambua na aliyedhamiria kuwa katika sehemu ya soko la muziki kwani aliujenga uwezo wake tokea akiwa na umri mdogo. Alizaliwa na baba mwanahabari na mwanadiplomasia. Vanessa alisomea mambo ya sayansi ya Sanaa katika jiji la Paris, Nairobi na kwao Arusha. Pia ameshiriki katika kazi za kujitolea kijamii na kufanya kazi na mashirika moja wapo: Staying Alive Foundation and ONE Mission. Mwaka 2013, Mdee alialikwa kuhutubia katika kongamano la Uchumi wa Dunia kwa Afrika katika mji wa Cape Town, Afrika ya Kusini.