STONEBWOY

COUNTRY OF ORIGIN : GHANA
GENRE : REGGAE, DANCEHALL

SOCIAL MEDIA

   

BIO

Stonebwoy ni msanii aliyefanikiwa kushinda tuzo ya msanii bora wa kimataifa kwa Afrika nchini Ghana. Mwaka 2015 alifanikiwa kushinda tuzo ya msanii bora wa mwaka, katika kipengele cha Reggae/Dancehall na Reggae/Dancehall wimbo bora wa mwaka. Hakika ni moja kati ya wasanii wenye vipaji vikubwa barani Afrika. Pia amewahi kutoa ngoma kali kama Go Higher na the remix to Pull Up ambayo alimshirikisha Patoranking. Stonebway ameendela kusafiri na kufanya matamasha mara kwa mara. Amewahi kushirikia na Haile Roots kutoka Ethiopia, mwaka 2016 ataonekana kwa mara ya kwanza katika msimu wanne wa Coke Studio

KAZI

Stobebwoy aliachia album yake ya kwanza iliokwenda kwa jina la “Grade 1 Album” chini ya Samini Music. Mafanikio ya album hii ndio iliyompa hadhi ya juu katika mziki wa Ghana. Mwaka 2015 alisign na VP Afrika. Album yake ya pili ni “Necessary Evil” imechaguliwa kuingia mara sita katika tuzo za muziki za Ghana.

MUZIKI

Kitu cha pekee kwa Stonebwoy ni style yake ya mziki. Uwezo wake umejikita kwenye uandishi na michano. Maepewa heshima ya kuwa mkali wa Ghana hivi karibuni. Stonebwoy alipatikana kutoka katika mashindano ya michano.

HISTORIA

Amezaliwa Livingstone Etse Satekla Ashaiman, Stonebwoy alianza kufanya mziki alipokuwa shuleni. Alisoma shule moja ya na mkali wa rap kutoka Ghana Sarkodie, na baadae akapata shahada yake ya masoko. Jina Stonebwoy amelipata akiwa shuleni ambapo alikuwa akirap kama msanii chipukizi. Alijizolea umaarufu baada ya kushindana katika “Kasahare Level” katika kituo cha radio cha Adom FM. Ameshirikiana na wasanii kama Sarkodie na Dr Cryme. Mashindano ya kurap ndio yaliyompa kibali cha kusainiwa na Samini Music. Chini ya hii lebo ndipo alipofanikiwa kurekodi ngoma yake kali inayoitwa Climax ambayo alimshirikisha Samini.