PATORANKING

NCHI ALIYOTOKEA: NIGERIAN
AINA YA MUZIKI: REGGAE, DANCEHALL

KURASA ZA KIJAMII

   

PATORANKING

Patoranking ni mshindi wa tuzo ya uimbaji kutoka Nigeria, mwandishi wa nyimbo na msanii mtumbuizaji anayejulikana sana kwa nyimbo yake ya Girlie O akimshirikisha Tiwa Savage. Nyimbo zake nyingine maaarufu ni kama Daniella Whine na Alubarika. Muziki wake ulioko katika miondoko ya reggae na dancehall umemfanya kuwa mmoja ya watumbuizaji wa kizazi kipya katika soko la muziki Afrika. Ataonekana katika msimu huu wa 4 wa Coke Studio Africa akishirikiana na malkia wa pop kutoka Tanzania, Vanessa Mdee.

 

KAZI

Mwaka 2015 alichaguliwa kama msanii wa mwezi wa MTV Base. Mwaka huohuo Patoranking alishinda tuzo ya MTV ya mwanamuziki bora wa kizazi kipya. Pia alishinda tuzo bora ya kizazi kipya ya City People Entertainment na tuzo ya Headies mwaka 2014 ya msanii anayechipukia-Tuzo yenye hadhi ya juu nchini Nigeria. Mwaka 2014, aliingia mkataba wa kurekodi na Foston Musik. Akiwa chini ya lebo hiyo alitoa nyimbo tano zilizokubalika. Katika harakati zake, ametumbuiza katika nchi ya Mauritius, New York, London na katika tamasha la Notting Hill akiwa na nyota wa muziki wa pop wa Marekani, Tinashe.

 

MASLAHI NA MUZIKI

Patoranking alipata umaarufu na kuibuka kuwa na mafanikio katika soko la muziki wa Nigeria shukrani kwa mchanganyiko wake wa kipekee wa dancehall, reggae na midundo yake ya kiafrika. Ameshatoa album aliyokuwa anaitarajia inayojulikana kwa jina la God Over Everything.

 

BACKGROUND

Patoranking ni wa mwisho kwenye familia ya watoto watano, amekulia katika makazi yanayojulikana kama Ilaje jijini Lagos, Nigeria. Familia yake iliishi katika umasikini uliokithiri hali iliyomlazimu Patoranking kuwa mchuuzi katika mitaa akiwa na umri mdogo. Alichukua hatua ya kujifunza muziki ili kubadilisha maisha yake na ya famila yake. Ajira yake ilianza kustawi pale tu alipoanza kufanya kazi na wasanii wakongwe kama vile XProject, Konga, Slam and Reggie Rockstone. Hit yake ya kwanza kutoka alishirikiana na Timaya kurekodi na kutoa kibao cha Alubarika-nyimbo inayojulikana kama “Baraka za Mungu”. Hii ni historia ya kweli  ya mabadiliko kutoka katika maisha ya geto mpaka kuwa shujaa-kutoka kwenye ufukara hadi kwenye neema.