KISS DANIEL

NCHI ALIYOTOKEA: NIGERIAN
AINA YA MUZIKI : Hip-Hop, Afro-pop

KURASA ZA KIJAMII

   

KISS DANIEL

Kiss Daniel ni mwimbaji kutoka Nigeria, mwandishi wa nyimbo, mtumbuizaji na mshehereshaji ambaye jina lake la halisi ni Anidugbe Oluwatobiloba ila anafahamika zaidi kwa jina lake la jukwaani. Nyimbo yake: Woju na Laye zilimpa umaarufu mkubwa. Ushirikiano wake na DJ Shabys katika nyimbo ya Raba ilikuwa ni moja wapo ya  ushirikiano bora kwake.

KAZI

Japokuwa Kiss Daniel hajawa katika soko la muziki kwa muda mrefu, ni dhahiri kusema kwamba yeye ni mfalme katika kizazi kipya cha wasanii Afrika. Mwaka 2015, Kiss Daniel aliachia albamu mpya ya New Era. Baada tu ya kuachia albamu mpya, albamu yake ilidumu kwa muda wa masaa 24 kwenye chati za muziki wa Marekani na masaa 48 katika chati za iTunes nchini Uingereza.

MASLAHI NA MUZIKI

Mwaka 2013, Kiss Daniel alisainiwa na lebo ya G-Worldwide Entertainment baada tu ya kuanza kazi yake ya muziki. Kati ya nyimbo zake za kwanza, video ya ngoma yake Woju ilikaa kwenye chati ya nyimbo kumi bora kwa wiki kumi na moja katika MTV Base Official Naija. Nyimbo yake iliyoimbwa na mwanamuziki anayeheshimika Nigeria nguli 2Baba iliwekwa mtandaoni. Hii ilithibitisha umaarufu na uwezo wa kipaji cha Kiss Daniel katika muziki.

HISTORIA

Kiss Daniel alionesha nia katika muziki akiwa na umri mdogo na kupata msaada kutoka kwa baba yake. Kwa hiyo fikiria kama Kiss Daniel asingekuwa mwanamuziki angejishughulisha na nini? Ana shahada ya uhandisi wa maji kutoka chuo cha kilimo cha Federal, Abeokuta.