EDDY KENZO

COUNTRY OF ORIGIN : UGANDA
GENRE : AFRO-BEAT, DANCEHALL

SOCIAL MEDIA

   

BIO

Eddy Kenzo ni mwimbaji kutoka Uganda ambaye ni msanii mwenye ushawishi mkubwa barani Afrika. Anashangiliwa kwa video yake inayoongoza kwa kutazamwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na ni mwanzilishi wa kikundi cha dansi cha watoto: Ghetto kids. Mwaka 2015 alishinda tuzo ya BET na kufuatiwa na nyimbo zilizovuma na kuweka jina lake katika anga za kimataifa. Nyimbo zake zilizovuma zaidi ukijumuisha Stimana na Yanimba. Miondoko yake ya midundo ya Afro ukichangana na dansi imemfanya kuwa kipenzi cha vijana wengi nchini Uganda wanaomtazama kama shujaa wao.

KAZI

Kufuatia tuzo aliyoshinda ya BET, Kenzo aliendelea kukusanya tuzo kadhaa za kimataifa ikiwemo ya msanii bora wa mwaka 2015 wa Nigeria, Video bora ya muziki katika tuzo za muziki Uganda mwaka 2015, matumizi bora ya kurasa za jamii tuzo ya muziki Hipipo mwaka 2015, tuzo ya video bora ya mwaka kutoka African Entertainment Marekani mwaka 2015, mwanamitindo bora wa kiume mwaka 2015 na tuzo nyinginezo.Katika harakati zake kimuziki pia ametumbuiza katika maonyesho ya SXSW 2015 Austin, Texas,Kombe la mataifa ya Afrika, Equatorial Guinea, Gabon, Ivory Coast ,USA ,UK na Cameroon.

MASLAHI NA MUZIKI

Eddy Kenzo kwa mara ya kwanza aliibuka nchini Uganda katika tansia ya muziki mwaka 2008 na nyimbo yake ya Yanimba.kufuatiwa na mafanikio ya kibao chake cha Stamina. Eddy alijulikana kimataifa mwaka 2014 baada ya kutoa kibao chake cha Sitya Loss,kilichoibua hisia na kutazamwa takribani mara 100,000 kwa siku na kuwa nyimbo iliyokuwa maarufu na kupendwa na wasanii maarufu kama Ellen Degeneres, P Diddy, Akon, Ronaldinho, Tevin Campbell, Sanaa Lathan na wengineo.

HISTORIA

Eddy Kenzo ni mwenyeji wa Uganda aliyezaliwa katika mji wa Masaka,Uganda kati.Katika umri wa miaka minne,Eddy alipoteza mama yake na kulazimika kuishi kama mtoto wa mtaani kwa Zaidi ya miaka kumi na tatu. Muziki ndio uliomuokoa na kubadilisha maisha yake.