CYNTHIA MORGAN

COUNTRY OF ORIGIN : NIGERIAN
GENRE : POP, HIP HOP, DANCEHALL, RAP

SOCIAL MEDIA

   

BIO

Mwanamuziki wa dansi kutoka Nigeria Cynthia Morgan wa nyimbo ya German Juice kwa mara ya kwanza atakuwepo  kwenye Coke Studio Afrika msimu wa 4 mwaka 2016. Katika msimu huu, atashirikiana na msanii kutoka Ethiopia Henok Mehari. Wote hawa wanasimamiwa na mtengenezaji  wa muziki Masterkraft. Mwimbaji/mwandishiwa muziki ,pop,hip hop,dansi na rap. Nyimbo zake zenye mafanikio ni pamoja na Come and Do, Popori, I’m Taken na Simatiniya.

KAZI

Katika umri wa miaka saba,Cynthia alianza kutunga muziki na alipofika umri wa miaka kumi na saba alirekodi nyimbo yake ya kwanza ujulikanayo kama Dutty stepping ambayo alimshirikisha General Pype.Baada ya hapo alisaini mkataba na Northside Entertainment Inc. inayomilikiwa na Jude Okoye, na hapo ndipo ajira yake ilipoibukia.

MASLAHI NA MUZIKI

Cynthia aliibuka kuwa maarufu kufuatia vibao vyake alivyoviachia: Don’t Break My Heart na Lead Me On. Vibao vyote vilipata umaarufu mkubwa na kupokelewa kwa mtazamo chanya na wakosoaji wa muziki. Nyimbo yake ya German Juice ndiyo iliyosambaa na kusikilizwa Zaidi.

HISTORIA

Cynthia Morgan alizaliwa katika jiji la Benin,mji wa Edo ambako ndiko alipomalizia elimu yake ya msingi. Katika umri wa miaka mitatu,tayari alikuwa msaidizi katika bendi ya mama yako. Aliamia katika jiji la Lagos mwaka 2008 ilikuendeleza kazi yake ya muziki.