BAHATI

NCHI ALIYOTOKEA: KENYA
AINA YA MUZIKI: GOSPEL

KURASA ZA KIJAMII

   

BAHATI

Mwanamuziki Bahati anaweka historia kuwa msanii wa kwanza wa injili kuneemeka Coke Studio Africa. Katika onesho la msimu huu wa nne, atashirikiana na msani mmoja chipukizi anayevuma kutoka Nigeria;Kiss Daniel. Akiwa kileleni mwa chati, Mama, Machozi na Wangu akishirikiana na Mr.Seed ndizo nyimbo alizofanikiwa kuzitoa.

 

CAREER  

Bila shaka Bahati ni mwanamuziki anayekuwa kwa kasi katika soko la muziki wa Kenya. Amekonga nyoyo za mashabiki na kufanikiwa kunyakuwa tuzo ya msanii bora wa Groove Awards–tuzo ya kiinjili yenye hadhi ya juu aliyoipata baada ya miezi saba tu kuingia katika soko la muziki. Pia alishinda tuzo ya AFRIMMA ya msaani bora wa kiinjili Afrika na nyinginezo.

 

MUSIC INTEREST

Mwaka 2010, alishiriki katika tamasha la muziki la kitaifa Kenya la shule za sekondari wakati anapiga gitaa. Safari yake ya muziki ilianza mwaka 2013 kwa kutoa nyimbo ya kwanza na video: Siku ya Kwanza. Alifanikiwa kupenya kwenye soko la muziki aliposhinda tuzo ya Groove Award mwaka 2013. Pia anaendesha studio yake ya kurekodi, inayosaidia vipaji vya muziki kutoka maeneo ya makazi duni.

 

BACKGROUND

Bahati alipatwa na uyatima katika umri mdogo na kuishia kuishi katika kituo cha watoto cha ABC childeren’s Home kilichopo Mathare. Bahati alivutiwa na mambo ya sanaa toka akiwa na umri mdogo. Alifanikiwa katika sanaa kwa kusoma mashairi ya Kiswahili shuleni na kanisani. Tangu afanikiwe katika muziki , Bahati pia amekuwa akijishirikisha na shughuli za kijamii. Anaendelea kufanya miradi inayowasaidia watoto walemavu katika makazi ya komarock nchini Kenya.