OMAWUMI

NCHI ALIYOTOKEA: NIGERIA
AINA YA MUZIKI: RNB, SOUL, AFRO-POP

 

KURASA ZA KIJAMII

   

Omawumi alianza rasmi kazi ya muziki mwaka 2007. Kuibuka kwake katika muziki kulianza kwenye mashindano ya Idol Afrika Magharibi. Kutokana na sauti yake nzito na umbo lake la kuvutia, alipigiwa kura kuwa msanii wa kwanza  mwenye mvuto  katika  shindano hilo.
Nje ya muziki, Omawumi mfanyabiashara. Hutumia muda wake wa mapumziko kuangalia TV kusoma riwaya zenye hadithi za matukio ya kihalifu, tamthilia na vitabu vya hadithi za kufikirika (Fantasy) na hujiburudisha kwa vinywaji vikali (cocktail).

Mwezi Septemba 2008, Omawumi alitoa single yake ya kwanza ilioitwa “In the Music” wenye sauti ya mahadhi ya kwaito ukichanganya na mahadhi ya kimagharibi. (Pidgin English) single iliyomfanya avume ghafla na ukachaguliwa na kushindania tuzo nyingi.
Albamu yake iliyokuwa inasubiriwa kwa muda mrefu ya “ WONDERWOMAN” ilitoka Novemba11, 2009. Albamu hii ilifanikiwa kuuza nakala 100,000 kwa kipindi cha wiki moja tu. 

Albamu yake ya pili iliyoitwa “ THE LASSO OF TRUTH” ilitoka Aprili 7, 2013, albamu ambayo ilitolewa katikati ya onyesho kubwa la muziki likiwashirikisha wasanii wakongwe kama Oyeka Onwenu, na Tuface Idibia. Pia, wasanii kama Timaya, Wizkid, Waje, na Tiwa Savage nao walishirikishwa. Aidha, Omawumi ni mtunzi wa nyimbo wa kiwango cha hali ya juu na mwimbaji mwenye nyimbo zenye sauti inayopanda juu wakati wa kuimba hasa anapokuwa akiimba kwa kushirikiana na wasanii wengine. 

Omawumi, anamhusudu sana, mwanamuziki Angelique Kidjo, mshindi wa tuzo inayotolwea nchini Marekani ya shindano la Benenoise, ambaye ni mtunzi mwimbaji na mhamasishaji. Anapenda miziki wake, uwezo wa sauti yake, uhodari wake na ukweli kwamba ni msanii wa kimataifa lakini amekuwa akithamini chimbuko lake. Iwapo Omawumi angefanya onyesho na msanii yeyote, popote pale, lazima angekuwa Angelique Kidjo hasa kwenye tuzo za Kimarekani. 

Kuhusu muziki wa Nigeria, anasema kuwa unakua na unaendelea kufanya vizuri. Omawumi anasema kuwa “Ningependa kukumbukwa kwa kuwa kujitambua kuwa mimi ni msanii na ni binadamu”.