OLAMIDE

NCHI ALIYOTOKEA :NIGERIA
AINA YA MUZIKI: RAP, RNB, NA HIP-HOP

 

KURASA ZA KIJAMII

   

Olamide Adedeji a.k.a Olamide, ni msanii wa Kinigeria kutoka kitongoji cha Bariga katika jimbo la Lagos anayerekodi muziki wa Hip-hop. Alitoa albamu yake ya kwanza ya ‘Rapsodi’ mwaka 2011 ambayo ilipokelewa kwa kishindo na mashabiki wake. Aliingia kwenye mkataba na studio maarufu ya Coded Tunes, mara baada ya kutoa albamu yake ya kwanza lakini albamu zilizofuata zilitolewa na label yake ya YBNL.

Olamide ni msanii ambaye kibao chake cha ‘Eni Duro’ kinachoibeba albamu yake ya kwanza, kilifungua njia ya kusonga mbele kimuziki. Hii ilimfanya aweze kufanya muziki na wasanii wengine kama vile Wizkid, ID Cabasa, 9ice, Reminisce, na D’banj, miongoni mwa wasanii wengine wengi. Single ya ‘Eni Duro’ ya Olamide uliongoza chati kwa kuombwa na mashabiki redioni.

Katika album yake ya pili, aliyoitoa kwenye studio ya YBNL ilitoka mwezi Novemba 2012. aliwashirikisha wasanii kama vile Davido, Tiwa Savage, KaySwitch, Dammy Krane, Reminisce, Samklef,Buckwylla, Minus 2, na Base One. Albamu hiyo ilichagizwa na vibao kama vile ‘Money’ ‘Owotabua’ ‘Fuji House’ ‘Voice of the Streets’ na ‘ Street Love’ pamoja na nyingine nyingi. Studio ya pili ya Olamide ilimfanya aonekane kuwa ni mwanamuziki aliyekomaa, na kuelewa vizuri soko lake la muziki na hakati tamaa katika kuhakikisha anaridhisha kiu ya washabiki wake. YBNL liliundwa na wasanii kama vile Tyrone, Samklef, 2Kriss, Pheelz na ID Cabasa.

Olamide alipoulizwa, kwa nini muziki? Msanii huyu anayevuma kwa Rap alijibu,”Niliona kuwa hiki ndicho kipaji changu, hivyo ilibidi niendelee kudadisi zaidi, ni maisha yangu, ni muzuka wangu, ni ulimwengu wangu”