NAVIO

NCHI ALIYOTOKEA: UGANDA
AINA YA MUZIK: HIP-HOP

 

KURASA ZA KIJAMII

 

Daniel Kigozi a.k.a ‘Navio’ ni kijana moto na mwenye kipaji cha muziki. Mara ya kwanza aliibukia kwenye muziki mwaka 2001 akiwa mmoja wa kundi la ‘Klear Kut’ kiisha akaanza kujitegemea kuanzia Machi 2008 na kuanzisha kampuni yake aliyoiita NavCorp Limited, kampuni mama ambayo kazi zote za Navio zinatayarishiwa.

Akiwa msanii wa kujitegemea, Navio alishinda Video Bora kwenye Tuzo za PAM mwaka 2007 na Msanii Bora wa Hip Hop mwaka 2008.
Uzinduzi wa albamu yake ya ‘Half the the Legend’ ulikuwa mkubwa kuliko shoo zote za hip-hop katika historia ya muziki wa Uganda. Ubora umekuwa ni tunu muhimu kwa mafanikio ya Navio  kama masanii na ndicho kitu ambacho alikitegemea hadi kufikisha anga za kimataifa kitu ambacho kwa hakika anakistahili.

Mara ya kwanza Navio kuingia studio na umri wa miaka10. Alipiga kinanda akiwa bado mtoto mdogo, lakini sauti yake ilikuwa silaha yake muhimu. Navio hutunga nyimbo zake mwenyewe kwa kuwa ana mistari mingi yaliyojaa kichwani mwake na msukumo wakutunga unatokana na hali ya maisha, ugumu wa maisha na wanawake! Kabla ya kupanda stejini, Navio hutaka kuona picha ya umati atakaoutumbuiza hivyo meneja wake hulazimika kupanda jukwaani na kupiga picha hiyo. Pia, huongea sala ya ma ‘gangstar’, haina chochote cha usanifu wala kufanyiwa maneno na ni vijineno vya hop-hop vimejaa humo. Wakati wa mapumziko, hupendelea kucheza basketball, kitu ambacho kipo moyoni mwake lakini pia huusikiliza muziki.